Rasimu ya ripoti ya muda ya wachunguzi wa Ethiopia imesema ajali mbaya ya ndege ya Boeing Max 737 iliyotokea tarehe 10 mwezi Machi mwaka jana 2019 na kuua watu 157 ilisababishwa na na matatizo ya kiufundi na ubovu wa ndege hiyo ya Kimarekani.

Eric Weiss, msemaji wa Bodi ya Taifa ya Usalama wa Usafiri wa Marekani (NTSB) amethibitisha kuwa taasisi kadhaa za usafiri na usafiri wa anga za Marekani zimepokea rasimu ya ripoti hiyo ya muda, kabla ya ripoti ya mwisho kutolewa.

Hata hivyo taasisi hizo za uchukuzi za Marekani zimekataa kulizingumzia suala hilo zilipohojiwa na waandishi wa habari.

Katika ripoti ya kwanza rasmi kuhusu ajali hiyo mbaya iliyotolewa na Ethiopia mwezi Aprili mwaka jana, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya ajali hiyo, serikali ya Addis Ababa ilithibitisha kwamba, marubani wa ndege hiyo ya Kimarekani ya Boeing MAX 737 ya shirika la Ethiopia Airline iliyoanguka nchini humo wakati ikiwa safarini kuelekea nchini Kenya, walifuata maelekezo yote ya kiusalama yaliyotolewa na shirika hilo la Kimarekani lililotengeneza ndege hiyo mbovu.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...