Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kikao na kamati ya Bunge ya Bajeti Mokoani Morogoro Leo March 6,2020.

…………………………………………………………………
Na Farida Said, Morogoro

Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepewa wasilisho juu ya maendeleo ya utekelezaji mradi Julius Nyerere (Mw 2115).

Wasilisho hilo limetolewa Mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa bwalo la JKT Umwema na kuhudhuriwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Saidi, Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.

Akizungumza baada ya wasilisho hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki alisema malengo ya kukutana leo na Wizara pamoja na TANESCO yalikuwa matatu.

Aliyataja malengo hayo kuwa ni kupata maelezo kutoka kwa Mhe. Waziri wa Nishati juu ya utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere tangu umeanza na hatua iliyofikia pamoja na kutembelea na kuona utkelezaji wa mradi.

“Tumejifunza kwamba mradi unaendelea vizuri na kwa kasi, kwa kazi zilizokuwa zimepangwa mpaka wakati huu zimefanyika kama zilivyopangwa na tunatarajia mradi utakamilika ndani ya muda uliopangwa Juni, 2022 “, alisema Mhe. Ndaki.

Aliongeza kazi ya kuchimba mtaro wa kuchepusha maji umekamilika na hatua mbalimbali zimefikiwa za ujenzi wa Bwawa.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kuhakikisha fedha zinalipwa lwa Mkandarasi kwa wakati.

Alisema Serikali ilitakiwa kulipa malipo ya awali kwa Mkandarasi aslimia 15 ambazo imeshazilipa kwa wakati.

Aliongeza Mkandarasi kila mpango kazi ambao upo kwenye mkataba wake amefikia takribani asilimia 85 za utekelezaji.

“Kazi ambazo zimekamilika Serikali imeshalipa fedha, na kwa ujumla wake kwa sasa Serikali imeshatoa fedha zaidi ya trilioni 1.19 na jumla ya fedha za utekelezaji ni trilioni 6.5 hadi kukamilika kwa mradi ambazo ni ufadhili wa Serikali kwa asilimia mia moja”, alisema Dkt. Kalemani.

Aliongeza utekelezaji wa mradi unakwenda vizuri ukiziangalia kazi kuu nne kama ujenzi wa “Power House”ambao ulitakiwa kuanza mwaka jana mwezi wa kumi, ulianza mwezi mmoja kabla.

Aidha kupitia utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere hadi sasa takribani Watanzania 3,642 wameajiriwa.

Kukamilika kwa mradi wa Julius Nyerere kutaifanya nchi kuwa na umeme mwingi, unaotabirika, imara na wa gharama nafuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...