Mkurugenzi wa Kampuni ya Smart Ndg. Remigius Nshange maarufu Dkt. Remmy akionesha utayari na maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona, mara baada ya kupatiwa mafunzo kutoka kwa maafisa Afya.
Afisa Afya Gabriel Zakaria kutoka Bukoba Manispaa akifundisha kwa vitendo namna ya kuosha mikono kwa sabuni wakati wa kuchukua tahadhali ya Ugonjwa wa Korona. 
Kituo cha Mafuta cha Smart Oil kilichopo Kibeta Bukoba Manispaa kama kilivyokutwa na Kamera yetu.


Wafanyakazi na wahudumu wa Kituo cha Mafuta cha Smart Oil wakiendelea na shughuli yao wakiwa tayari wamevalia viziba pua (mask) kwa kuchukua tahadhali ya Korona.

Wafanyakazi na wahudumu wa Kituo cha Mafuta cha Smart Oil wakiendelea na shughuli yao wakiwa tayari wamevalia viziba pua (mask) kwa kuchukua tahadhali ya Korona. 
Wafanyakazi na wahudumu wa Kituo cha Mafuta cha Smart Oil wakiwa tayari wamevalia viziba pua (mask) kwa kuchukua tahadhali ya Korona. 


Na Abdullatif Yunus - Michuzi TV


Wananchi Taasisi na Makampuni mbalimbali hapa Nchini wameendelea kuchukua tahadhali juu ya Ugonjwa wa Korona ambao unazidi kuyanyemelea mataifa jirani na Tanzania ikiwa tayari ugonjwa huo umebisha hodi Nchini Kenya.



Miongoni mwa makampuni hayo yaliyoanza kuchukua tahadhali hiyo ni pamoja Kampuni ya Smart ya Mjini Bukoba Mkoani Kagera ambayo inaundwa na Vituo vya Mafuta vya Smart Oil, Smart Hotel, maduka ya Jumla ya Dkt. Remmy pamoja na wakala wa bidhaa za Mukwano toka nchini Uganda, ambapo wafanyakazi wake wamepatiwa semina fupi kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya korona pindi wanapowahudumia wateja wao.



Akizungumza muda mfupi kabla ya mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Smart Ndg. Remigius Patrick Nshange maarufu kama Dr. Remmy amesema kufuatia Nchi kuwa katika tahadhali kubwa Ugonjwa huo, ameona ni vyema wafanyakazi wake wakapewa mafunzo hayo stahiki, ili kutambua viashiria vya Ugonjwa na kujikinga hasa pale wanapotoa huduma zao kwani Kampuni ya Smart inahudumia watu tofauti mataifa mbalimbali.



Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika Kituo cha Mafuta cha Smart Oil, yakifundishwa na Afisa Afya kutoka Manispaa ya Bukoba Gabriel Zakaria, akiambatana na Bibi Afya wa Kata Kibeta Salima Kayanda, yamewahusisha wafanyakazi zaidi ya 50, pamoja na wateja wao waliosimama kwa muda kunufaika na Elimu hiyo.



Haya yanajili wakati ambapo Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli ameendelea kuhimiza Taifa kuchukua Tahadhali na kinga ni bora kuliko tiba, na Kwa Bukoba tayari Smart ni Kampuni ya kwanza ambao wameanza kutekeleza agizo hilo tukiamini wengine watafuata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...