Nchi za Afrika za Kenya, Ghana na Gabon zimetangaza kuwepo kesi za watu walioambukizwa ugonjwa wa COVID-19 au corona katika kile kinaachoonekana ni kuenea ugonjwa huo hatari duniani.

Wizara ya afya ya Ghana imesema watu waliorejea kutokea Uturuki na Norway wamepatikana na corona. Naye Waziri wa mawasiliano wa Gabon Edgard Miyakou ametangaza kuwa mtu mmoja amethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini humo. Serikali ya Gabon imesema aliyeambukizwa ni kijana mwenye umri wa miaka 27 raia wa Gabon ambaye amerejea kutoka Ufaransa Machi 8.

Mapema leo Ijumaa , Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe amesema kesi ya kwanza ya corona imebainika katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Amsema mgonjwa huyo ni mwanamke ambaye amesafiri kutoka Marekani akipitia London kabla ya kuwasili Nairobi.
 
 Amesema mgonjwa huyo ni raia wa Kenya na hali yake imeanza kuboreka lakini hataruhusiwa kuenda nyumbani hadi apone. Mwanamke huyo amelazwa katika kitengo maalumu cha corona katika Hospitali Kuu ya Kenyatta mjini Nairobi. Serikali ya Kenya imesema inawafuatilia wale wote aliokuwa amekaa karibu nao ndani ya ndege ili kubaini iwapo amewaambukiza.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...