Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi anawataarifu
Maafisa Habari na
Mawasiliano Serikalini pamoja na wadau wengine kuwa Kikao Kazi kilichotarajiwa
kufanyika tarehe 9 hadi 13 Machi 2020, Jijini Mbeya kimeahirishwa.
Kikao
kazi hicho ambacho hufanyika kila mwaka ili kuwajengea uwezo Maafisa Habari na
Mawasiliano wa Serikali namna ya kutangaza shughuli za Serikali na kuhakikisha,
Idara na Vitengo vya Mawasiliano na
Uhusiano Serikalini vinaimarishwa ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya
Tano na Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano katika kuwahudumia wananchi.
Aidha,
Maafisa hao wametakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yao katika
maeneo ya kazi kwa kutangaza utekelezaji
wa Serikali ili wananchi waweze kupata taarifa muhimu za Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...