Wachezaji
wa timu ya Dar es Salaam Corridor Group (DCG) ya Tanzania wameahidi
kuwa mabalozi wazuri wa soka baada ya mafunzo waliyopata kutoka kwa
makocha wa Liverpool.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered Tanzania yaliwahusisha wachezaji sita ambao walikuwa chini ya gwiji wa zamani wa timu ya Liverpool John Aldridge.
Wachezaji hao ni Salim Kuziwa, Michael Lyimo, Rafael Kutoka, Yusuph Lugonzo, Godfrey Waninda na Abdallah Maguzo.
Nahodha wa DCG, Raphael Kutoka alisema kuwa wamepata hamasa kubwa katika mafunzo hayo kwani wamezaliwa upya.
Kutoka alisema kuwa bado wana umri wa kucheza mpira wa ushindani na wanaamini watakaporejea watatumia ujuzi waliopata na hamasa kucheza mpira wa ushindani mbali ya majukumu yao ya kazi ya kila siku.
“Kwa kweli tumefungua macho, tumeona jinsi wachezaji wa Liverpool wanavyoandaliwa tokea wakiwa wadogo,kwa miundombinu hii, lazima timu ipate mafanikio, tunaishukuru benki ya Standard Chartered kwa kutimiza ndoto zetu na kupata uzoefu ambao huwezi kununua kwa kiasi chochote cha fedha,” alisema Kutoka.
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered Juanita Mramba alisema kuwa wanajisikia faraja kutimiza ahadi yao kwa kuwasafirisha washindi wa mashindano yao wa mwaka jana.
Mramba alisema kuwa benki yao itaendelea kusapoti maendeleo ya michezo na sekta nyingine kupitia sera zao.
“Tumetimiza ahadi yetu na wachezaji wa timu ya DCG wamepata mafunzo kutoka kwa Aldridge na vile vile kutembelea uwanja wa Anfield na kuona mechi dhidi ya Bournemouth ambapo Liverpool ilishinda kwa mabao 2-1," alisema Mramba.
" Tunaamini wachezaji wamejifunza mengi na watakuwa walimu wazuri kwa wenzao na kuhamisika kucheza na kuleta matunda mazuri ya maendeleo ya soka nchini Tanzania,” aliongeza Mramba ambaye ameambatana na Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Lucia Damas.
Wachezaji
Dar es Salaam Corridor Group wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered Tanzania wakati wa mechi ya
Ligi Kuu ya England kati ya timu ya Liverpool na Bournemouth iliyochezwa
kwenye uwanja wa Anfield jana. Liverpool ilishinda mabao 2-1.


Wachezaji
wa timu ya Dar es Salaam Corridor Group wakimsikiliza gwiji wa
Liverpool ambaye ni kocha wa Academy John Aldridge (kulia).


Wachezaji wa timu ya Dar es Salaam Corridor Group wakiwa katika picha ya pamoja na kocha wa Academy John Aldridge (kulia)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...