Na Avila Kakingo-Michuzi Blog

MAKATIBU wakuu na Manaibu  wa Wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli wameshangazwa na maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa ya Umeme (SGR).

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa Mradi wa reli ya Kisasa kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma, amesema kuwa kwakuwa mradi huu unazungumzwa katika vikao vyao ndio mana leo wamefanya ziara katika mradi huo.

"Leo tumekuja kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika eneo hili la mradi ambapo tunaona mradi unaenda vizuri kabisa."

Licha ya hivyo Reli ya kisasa itapita katika madaraja pamoja na Mahandaki ambayo yanaendelea kujengwa na Kampuni ya Yapi Markezi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa sekta ya Uchukuzi, katika Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamriho amesema kuwa kufikia Januari hadi mwishoni mwa Februari ni kiwango kizuri ujenzi utamalizika kwa wakati.

"Kufikia Mwezi Januari mwaka huu makandarasi walikuwa wameshafanya kazi kwa asilimia 25.8 hadi mwishoni mwa februari walikuwa wamefikia asilimia 28 kwa hiyo hicho kiwango ni kizuri tutamaliza kwa wakati."

Hata hivyo Makatibu wakuu na manaibu walitembelea mradi huo kwa kupita katika barabara inayotumika kujenga reli hiyo kuanzia jijini Dodoma hadi kufikia Mkoa wa Morogoro.
 Makatibu wakuu wakiingia katika Handaki.
 Katibu mkuu wizara ya Elimu, Avemaria Semakafu akijipiga selfii kwenye reli ya kisasa ya umeme

 Picha ya pamoja.

 Muonekano wa Handaki.
Makatibu wakuu na makatibu wakuu wa wizara mbalimbali wakiwa katika picha ya maoja mara baada ya kuingia katika handaki yenye urefu wa kilomita 1.03.
 Muonekano wa Reli ya kisasa kwa maeneo yaliyokamilika mkoani Morogoro
 Makatibu wakuu wakipata maelekezo mara baada ya kufika katika eneo ambalo ujenzi unaendelea kwa uwekaji wa Mataluma
 Makatibu wakuu na manaibu wakipata maelekezo mara baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza mataluma.
 Makatibu wakuu na manaibu wakitoka katika handaki
 Eneo ambalo ujenzi unaendelea na nguzo za umeme zimewekwa kama inavyoonekana.
 Ujenzi ukiendelea
 Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa akizungumza na makatibu wakuu na Manaibu Waziri walipotembelea mradi wa Reli ya kisasa ya Umeme ya SGR
 Makatibu Wakuu wakipata maelekezo walipopita katika ujenzi wa reli ya zamani ambayo iliharibika baada ya mto Mkondoa kujaa maji.
Makatibu wakuu na manaibu wa wizara mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika eneo ambapo litachombwa Handaki jingine kama inavyoonekana mduara wa nyuma ndipo litakapo chimbwa.Picha zote na Avila Kakingo-Michuzi Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...