Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Sweetbert Njewike |
Na Ismail Luhamba, Singida
JESHI la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tuhuma za kusamabaza taarifa za uongo kuwa watu 14 Wilayani Manyoni walifariki kwa kuchinjwa katika matukio mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Sweetbert Njewike (pichani kulia) alisema wamemkamata Mbunge huyo jana tarehe 2 na tayari wamemleta mkoani hapa kwa mahajiano zaidi na baada ya mahojiano atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Siku chache Jeshi hilo lilimfungulia jalada la uchunguzi Mbunge huyo wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema kufutia kutoa taarifa za uongo kuwa watu 14 wilayani Manyoni mkoani hapa walifariki dunia kwa kuchinjwa katika matukio mbalimbali wakati alipokuwa kwenye mazishi ya Alex Jonas ambaye mwili wake ulikutwa umetupwa na kukatwa katwa sehemu mbalimbali za mwili wake katika eneo la mbugani wilayani humo.
“Tumemkamata Mbunge huyu kutokana na kauli na taarifa aliyoitoa febrali 29 mwaka huu kuwa watu 14 wote waliuawa kwa kuchinjwa Wilayani Manyoni taarifa ambazo sio za kweli," alisema Kamanda Njewike
Awali kabla ya kukamatwa kwa mbunge huyo Kamanda Njewike aliwaambia Waandishi wa Habari kuwa taarifa iliyotolewa na Mbunge huyo ni ya uongo yenye lengo la kuleta uchochezi na taharuki kwa wananchi kwani matukio yote ya mauaji yaliyotolewa na Mbunge huyo yametokana na wizi,wivu wa kimapenzi na migogoro ya kifamilia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...