Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema yumkini asilimia 60 hadi 70 ya jamii ya nchi hiyo ya Ulaya itaambukizwa virusi vya Corona.

Merkel alisema hayo jana Jumanne mbele ya Bunge la nchi hiyo ambalo lilipokea kwa mshtuko mkubwa takwimu hizo za kuogofya za Kansela wa nchi hiyo.

Amesema ikilazimu, vikao vya Bunge la nchi hiyo ya Ulaya vitasimamishwa, sambamba na kufutwa kwa mikutano na shughuli zenye mijumuiko ya watu wengi. Hata hivyo hajaeleza serikali yake imejiandaa vipi kukabiliana na mripuko wa Corona, iwapo hali itazidi kuwa mbaya nchini humo.

Kufikia sasa, Ujerumani ina kesi 1,400 za ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, huku watu wawili wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo nchini humo.

Italia ndiyo nchi ya Ulaya iliyoathirika zaidi na Corona, kwani kufikia sasa watu 631 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo nchini humo, huku waliombukizwa wakiwa zaidi ya elfu 10.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...