NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
Shule ya sekondari Mwambisi ,Kongowe Kibaha mkoani Pwani ,imebuni mradi wa ufugaji nyuki na mizinga kwa ajili ya asali ili kujipatia kipato pamoja na kufundisha wanafunzi somo la stadi za maisha kupitia mradi huo.

Aidha shule hiyo, inatunza mazingira kwa kupanda miti maeneo ya shule na kuotosha miche ya miti mbalimbali ambapo kwa mwaka huu wameotesha miche 10,000.

Akizungumzia ubunifu huo ,mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mwambisi Joseph Simba alisema ,kwasasa wana mizinga kumi na mingine miwili ina asali tayari.
 "Mizinga hii tulipatiwa na mdau wa masuala ya mazingira na elimu Ibrahim Mkwiru, huyu mdau anatufadhili mambo mengi shuleni hapa, na alituletea wataalamu ambao walitupatia mafunzo ya namna ya kufuga na kulinda mizinga hii"utaalamu huu sasa unatuwezesha kutoa ujuzi kwa shule nyingine jirani ambazo huenda kujifunza ufugaji wa nyuki na mizinga .

"Wanafunzi wanatakiwa kujifunza kwa vitendo ,kulinda vyanzo vya maji,kutunza mazingira na kuboresha mazingira ili kuzuia kuondoa uoto wa asili,kwa manufaa ya vijazi vijavyo"alifafanua mwalimu Joseph.

Hata hivyo ,pia wameanzisha vyanzo vya maji ambavyo vinasaidia katika ulinzi wa mazingira na jamii inayowazunguka kuchota maji wakati yakikatika.
 Akielezea changamoto za shule, alisema ina madarasa 14 mahitaji ni 25 na pungufu ni vyumba tisa, hakuna kabisa nyumba za walimu na jengo la utawala na upungufu wa madawati 160 na walimu wa sayansi nane.

Kwa upande wake ,Mwanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo,Zainab Sultan alielezea, miti inawasaidia vivuli ,kupendezesha shule ,kuleta mvua na kuepusha uoto wa asili.

Nae mdau wa mazingira Ibrahim Mkwiru alisema, amejikita na utaalamu huo na hadi sasa ameshatoa mizinga kwenye vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na wafugaji wadogo wa nyuki ili kufuga na kujiongezea kipato.
Mkwiru alifafanua, ameungana na baadhi ya wataalamu wa nchi za nje katika masuala ya mazingira ambao huwa wakija hasa eneo la Kongowe na kwingine kutoa elimu ya mazingira na nyuki kwa manufaa ya jamii.

Shule ya sek Mwambisi ilianza mwaka 2014 ikiwa ilianza na wanafunzi 84 na kufikia sasa ina wanafunzi zaidi ya 800.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...