Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru ( aliyenyoosha mkono) akikagua leo ujenzi wa jengo la Mahakama Jumuishi la Utoaji Haki (IJC) lililopo eneo la Kihonda Wilaya ya Morogoro. Jengo hilo linajumuisha Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya zikiwemo ofisi za wadau wote wa Mahakama.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (wa pili kulia) akizungumza leo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loatha Sanare kuhusu ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kukagua ujenzi wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.
Mafundi wakiendelea na ujenzi leo wa jengo la Mahakama Jumuishi la Utoaji Haki (IJC) lililopo eneo la Kihonda Wilaya ya Morogoro. Jengo hilo linajumuisha Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya zikiwemo ofisi za wadau wote wa Mahakama.
(Picha na Magreth Kinabo – Mahakama)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...