Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambaye ameitembelea Iran hivi karibuni amepongeza juhudi kubwa za vyombo na taasisi za afya hapa nchini katika kupambana na virusi vya Corona.

Dr. Christoph Hamelmann ameashiria ziara na ukaguzi wake akiwa pamoja na wataalamu kutoka China katika hospitali na taasisi za afya nchini Iran na kusema: Wataalamu wa China wameathiriwa sana na huduma zinazotolewa katika hospitali hizo.

Mwakilishi wa WHO amesema kuwa, kuwepo vituo bora na madhubuti vya huduma za awali za afya nchini Iran ni suala muhimu sana ambalo limewaathiri na kuwagusa sana wataalamu waliotembelea vituo hivyo.

Dr. Hamelmann amesisitiza kuwa, Iran ina moja kati ya mifumo imara zaidi wa afya katika eneo la magharibi mwa Asia.

Wakati huo huo wataalamu nchini Iran wako mbioni kutengeneza chanjo ya kirusi cha Corona aina ya COVID-19 na inatarajiwa kuwa watatangaza mafanikio yaliyopatikana katika uga huo katika siku zijazo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...