Naibu waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira na wenye ulemavu Mhe. Antony Mavunde,amewataka watumishi wa Wakala wa Usalama na afya Mahali Pa Kazi (OSHA) kuendelea kufanya kaguzi na kuendelea kuwaelimisha jamii kuhusiana na mambo mbalilmbali yahusuyo Usalama na Afya kwa wafanyakazi, kwani kutasaidia kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi.

Hayo yamesemwa Jijini Arusha wakati wa ukifunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Mhe. Mavunde amesema nguvu kazi kubwa itategemea juhudi zetu katika kuhakikisha kuwa Usalama na Afya unakuwepo muda wote.

Mhe.Mavunde, amesema OSHA ni taasisi hii ni muhimu katika ustawi wa ujenzi wa uchumi wa Viwanda nchini, kwani kutasaidia jamii yetu hususani Vijana kulinda usalama na afya zao . Ameipongeza OSHA kwa kuongeza juhudi za ukaguzi na  hivyo kupunguza malalamiko kwa wadau wake, amesema OSHA isipotimiza wajibu wake  kutasababisha madhara makubwa  kwa wafanyakazi kwa kuathiriwa na magonjwa na ajali sehemu za kazi.
 Naye kwa upande wake Kaimu Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi(OSHA) Bi Khadija Mwenda amesema  Katika mpango mkakati wa taasisi wa miaka 5 unalenga kuongeza ukaguzi  ili maeneo ya kazi mengi yaweze kukidhi viwango vya usalama na afya na hivyo kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi

Bi.Mwenda amesema katika Kipindi cha Miaka 5 waliofanya utafiti imeonyesha ya kuwa ajali sehemu za kazi zimepungua kutoka ajali 339 kwa mwaka 2018 hadi ajali 128 mwaka 2019,  katika utafiti huu uliofanyika katika mikoa 5 ya Dar es salaam,Mwanza,Arusha,Morogoro,Dodoma,Mtwara na Mbeya ,Sekta ya Uzalishaji inaongoza kwa kusababisha ajali  840 ikifuatiwa na sekta ya Ujenzi ajali 153.
 Awali akimkaribisha Mgeni rasmi kufungua Baraza hilo ,katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu ndugu Andrew Massawe, amesema OSHA imekuwa msaada katika kuhakikisha  kuna kuwepo na utekelezaji wa sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi, na Kuwenga mazingira.
 Naibu waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira na wenye ulemavu Mhe. Antony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Wakala wa Usalama na afya Mahali Pa Kazi (OSHA) wakati wa ukifunguzi wa Baraza la Wafanyakazi hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...