BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeanzisha mfumo mpya wa usajili kwa njia ya mtandao( MEMS) kwa wanafunzi, wanachama na wadau wake ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo imeeleza kuwa mfumo huo unatoa fursa kwa wanafunzi na wanachama kupata huduma mbalimbali  zinazotolewa na Bodi ikiwa ni pamoja na kufanya usajili, kufanya malipo mbalimbali, kuhudhuria semina, kununua vitabu na kadhalika kupitia mtandao.

Kuhusiana na namna ya kujisali imeelezwa kuwa mtahiniwa au mwanachama atatakiwa kutembelea tovuti ya Bodi ambayo ni http://www.nbaa.go.tz/ na kuendelea kwa  kubonyeza kitufe cha usajili na kuchagua chaguo la mtahiniwa au mwanachama.

Aidha imeelezwa kuwa mwanachama au mtahiniwa atatakiwa kuwa na jina pamoja na nywila;

"Katika usajili mtahiniwa anatakiwa kuweka jina la mtumiaji na nywila na ataanza kwa kuandika cr au ga/acpa na kufuatiwa na namba yake ya usajili na nywila yake ambayo anaweza kuibadili kwa ulinzi wa taarifa zake" imeeleza taarifa hiyo.

Kwa wanachama na watahiniwa wapya watatakiwa kujaza fomu maalumu katika tovuti hiyo kwa kubofya kitufe cha sajili sasa "Register Now" na kujaza taarifa katika fomu maalumu kama ilivyoandikwa kwenye vyeti vya taaluma.


Kwa maelezo zaidi soma hapa chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...