BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imesitisha utoaji wa mafunzo yaliyopanga kufanyika kuanzia Machi 18 mwaka huu na kuwataka wadau kusubiri hadi pale itakavyopangwa tena.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bi Shamim Mdee, Afisa mwandamizi masoko na uhusiano kwa umma wa Bodi hiyo imeelezwa kuwa kusitishwa kwa mafunzo hayo kumetokana na tamko rasmi la Serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzuia uwepo wa mikusanyiko ya watu katika maeneo mbalimbali nchini na hiyo ni mara baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa maambukizi ya virusi ya Corona (Covid 19) ambapo hadi sasa visa vitatu vimeripotiwa nchini.
Bodi hiyo imewataka wadau na wananchi kwa ujumla kufuata taratibu zilizowekwa katika harakati za kupambana na maambukizi na hiyo ni pamoja na miongozo ya afya iliyotolewa na Wizara husika ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na kuepuka kushikana mikono kwa kipindi hiki ambacho maambukizi ya virusi vya Corona (Covid 19) yanashika kasi kote duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...