Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmed Ahmed anatarajia kuwasili nchini Siku ya Jumamosi Machi 7 kwa mwaliko wa Rais wa TFF.
Ahmad anakuja nchini kwa kwa mara ya kwanza na ataishuhudia mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itakayochezwa Jumapili Machi 8, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa CAF kupata nafasi ya kuja nchini na kushuhudia mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayowahusisha watani wa jadi Yanga na Simba.
Rais huyo atawasili Jumamosi na kuondoka Jumanne kurudi kwao Madagascar.
Mchezo wa watani wa Jadi unasubiriwa kwa hamu kubwa na ni mechi inayotazamwa na mashabiki wengi na ya pili kwa ukubwa Afrika.
Katika mchezo wa awali, timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 2-2 mechi iliyipigwa January 04 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...