Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John ombe Magufuli amemnusuru mbunge wa Iringa Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA Peter Msigwa Kutoendelea kutumikia kifungo cha Miezi mitano ama kulipa faini ya sh. Milioni 40 alichohukumiwa juzi Machi 10 2020 baada ya kumlipia faini ya sh milioni 38 kati ya milioni 40.
Hatua hiyo imefikiwa leo Machi 12,2020 baada ya familia kwenda kuomba msaada kwa Rais Magufuli kufuatia wao kuchangishana na kufanikiwa kupata sh. Milioni mbili tu na kushindwa kutimiza fedha zilizobakia.
Akizungumza nje ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo hukumu hiyo ilisomwa, kaka yake mkubwa na mchungaji Msigwa, mchungaji Benet Simon Msigwa amesema tangu jana wamekuwa kwenye kampeni kubwa ya kutafuta fedha ili kumnusuru na adhabu iliyokuwa ikimkabili mchungaji Msigwa na wamefanikiwa.
"Tunashukuru sana mheshimwa Rais kwa ukarimu wake aliotufanyia maana tulikuwa tumekwama.
Mimi ni 'Kayemba' mjomba wangu ameoa binti yake Rais
Mbunge Peter Msigwa alihukumiwa kifungo hicho baada ya yeye na viongozi wenzake nane wa CHADEMA akiweno Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kukutwa na hatia katikanmashtaka 12 kati ya 13 yaliyokuwa yakiwakabili.
Baada ya kusomewa adhabu zao Msigwa yeye alihukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 40 ama kwenda jela miezi mitano.
Katika mashtaka yake Msigwa anadaiwa Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam akiwa na wenzake hap walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko kutawanyika.
Katika mashitaka ya pili inadaiwa kuwa Februari 16,2018 katika ya viwanja vya buibui na Mwananyamala Kinondoni washtakiwa hao wakiwa wamekusanyika na adhma ya pamoja, waliitekeleza kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope kuwa watakwenda kupelekea vunjïfu wa amani.
Katika mashitaka ya tatu, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Februari 16,2018 walifanya mkusanyiko wenye ghasia, wanadaiwa kuwa siku hiyo katika viwanja vya Buibui Mwananyamala na barabara ya Kawawa Kinondoni kwa pamoja na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walitekeleza mkusanyiko ama maandamano yasiyo halali wakiwa na lengo la kuvamia ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kuĺeta hofu ya uvunjifu wa amani.
Pia Februari 16,2018 katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washtakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la afisa wa polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani ambao ulisababisha hofu na hatimaye kifo cha Akwilina na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.
Katika mashitaka ya 12 ya kushawishi utendaji wa kosa la jinai, linamkabili Msigwa, peke yake ilidaiwa katika maeneo hayo hayo Msigwa anadaiwa kushawishi Raia na wakazi wa eneo hilo kutenda kosa la jinai kwa kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha

Kaka michuz mbona vijana wa op magufuli wenye shahada hawajaajiriwa wote wakati kupitia blog yako katibu alisema wote wataotuma cv zao wataajiriwa lakini sivyo wengine wameitwa wengine hawajaitwa kupangiwa nafasi za kazi na usaili walifany wote...tunaomba ufanye mahojiano na katibu mkuu mh.ndumbaro kumuulzia tamko rasmi alilotoa rais mbona hajarikamilisha
ReplyDelete