RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kiasi cha shillingi Billioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyojengwa kwa miaka 40 bila kumalizika.
Haya yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi katika hospitali hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi wake.
Akizungumza mara baada ya kutembelea Hospitali hiyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Hospitali hiyo itakuwa masaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara hasa kwa huduma za matibabu ya kibingwa.
"Kutakuwa hakuna haja ya kwenda Hospitali ya Kanda Bugando kupata matibabu ya kibingwa kwani tunataka huduma za kibingwa zitolewe hapa hapa"alisema
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Shirika la Nyumba na Chuo Kikuu cha Ardhi kimepewa kazi ya kusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo hivyo ameagiza kazi kufanyika usiku na mchana ili limalizike kwa muda uliopangwa.
"Tumekubaliana tarehe 17 mwezi huu wa tatu wawe wamekamilisha Wing C ili huduma za Mama na mtoto zinanze kutolewa kwa muda husika" alisema
Kwa upande wake Mkuu Mkoa wa Mara Adam Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia hospitali hiyo iliyokwama kwa muda wa miaka 40 mpaka sasa.
“Hospitali hii imechukua awamu tano za marais kumalizika na tunamshukuru Rais kwa kuchukulia kipaumbele katika hili” alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...