Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya  kamati ya watu 13 kutoka Serikali na sekta binafsi ambao watapitia mikataba yote ya miradi mbalimbali iliyosainiwa mkoa wa Dar es salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa globu ya jamii)

* RC Makonda asema hakuna mgonjwa wa Covid 19, awataka wananchi kufuata maelekezo

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza kamati ya watu 13 kutoka Serikali na sekta binafsi ambao watapitia mikataba yote iliyosainiwa jijini Dar es Salaam na kushauri nini kifanyike na hiyo ni pamoja na kuweka wazi mikataba yote ya utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo iliyosainiwa ili wananchi waweze kutambua ni nani anakwamisha utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ni muhimu kwa kwao lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasusa kwa kiwango kikubwa.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya katika Mkoa hasa kwa wakandarasi wanaoshinda tenda za utekelezaji wa miradi mbalimbali lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasusa na kuchelewa.

"Licha ya kuwakamata na kuwaweka ndani bado kuna mikataba iliyosainiwa na pesa zimetolewa ila miradi haiendi, kwa mfano mto Ng'ombe mkandarasi amepewa zaidi ya bilioni nne lakini hadi sasa mradi umefika asilimia 6 tuu huku akitumia asilimia 60 ya muda wake" Ameeleza Makonda.

Amesema kuwa  timu hiyo ya watu 13 kutoka serikalini na sekta binafsi  watashauri nini kifanyike ikiwemo kuhakikisha mikataba inawekwa wazi, ili kila mwananchi ajue mkataba umesainiwa na nani, anayesimamia ni nani pamoja na muda wa utekelezaji hali itakayowasaidia wananchi kufahamu nani anakwamisha utekelezaji wa mikataba hiyo.

Amesema hadi sasa mikataba yote imekusanywa na baada ya kamati hiyo kukaa na kujadili mikataba isiyo na tija na baaifu itavunjwa kisheria.

Kuhusiana na mlipuko wa virusi vya Corona (Covid 19) Makonda amesema wananchi wafuate mwongozo uliotolewa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu na amewataka wananchi wa Mkoa huo kutokuwa wabishi pindi wanapopewa maelekezo ya namna ya  kujikinga na virusi hivyo.

" Tuzingatie usafi na namna ya kusalimiana, nashauri tutumie teknolojia ya mitandao ya kijamii kwa umakini hasa kwa kutosambaza taarifa zenye kuleta hofu ya ugonjwa wa Corona, ukiona hali ya dalili toa taarifa na hatua stahiki zitachukuliwa"

Amesema kuwa Serikali ipo makini na hadi sasa hakuna aliyegundulika kuwa na  virusi hivyo na amewaomba viongozi wa dini kuendelea kukuweka taifa kwenye maombi ili tuweze kulivuka janga hilo lililoikumba dunia.

Katika hatua nyingine RC Makonda amezitaka wakala za barabara za TANROAD na TARURA kurejesha miundombinu yote kwa kuwa kuwa fedha za marekebisho takribani shilingi bilioni 165 zimekwishatolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...