Na Shukrani Kawogo, Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ametoa wito kwa wanawake nchini kubadilika kifikra na kimtazamo ili kufikia usawa wa kijinsia katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Ole Sendeka aliyasema hayo alipokuwa akizindua wiki ya siku ya mwanamke duniani mkoani Njombe ambapo alisema taifa linahaki ya kujivunia kwa kuwa na wanawake wenye nafasi kubwa ndani na nje ya nchi hali ambayo nchi nyingi hazijafikia.
Alisema kuwa mkoa wa Njombe ni kati ya mikoa nchini ambayo imekuwa ni vinara wa kilimo cha mazao mbalilmba yakibiashara hivyo ni vyema wanawake mkoani Njombe wakakubushwa kujikita katika kilomo ili kujikwamua kiuchumi.
Aidha amewataka wanawake mkoani Njombe kuchangamkia fulsa yakugombea katika nafasi za udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020.
Ole Sendeka alisema ongezeko kubwa la wanawake ndani ya bunge la jamhuri ya muungano kuwa ni uwiano sawa katika nyanja zote ni jambo la kujivunia sana hapa nchini.
"Katika miimili hii mitatu ya nchi,ni idadi isiyopungua asilimia 80 ya wabunge wanawake katika bunge la jamhuri ya muungano Tanzania wakati fulani tulikua na majaji wa mahakama kuu zaidi ya asilimia 40 walikua wanawake"alisema Sendeka.
Siku ya mwanamke duniani inatarajiwa kufanyika march 8 ambapo mkoani Njombe siku hiyo inatanguliwa na matukio mbalimbali ndani ya wiki hiyo lengo ni kujali,kuthamini na kuunga mkono mchango wanawake nchini.
Ufunguzi huo umefuatiwa na shughuli za kijamii kwa kuwatembelea wagonjwa na kutoa zawadi mbalimbali katika wodi ya wanawake hospitali ya Mji Njombe Kibena.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...