NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MAKAMU
 wa Rais na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu pamoja na 
Rais mstaafu Jakaya Kikwete  wameungana na wadau , kwenye harambee ya 
kuchangia zaidi ya sh.milioni 500 ili kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa 
CCM mkoani Pwani,":ambapo ameeleza chama hicho mkoa sio maskini badala 
yake waviendeleze vitega uchumi walivyonavyo.
Katika
 harambee hiyo, imeweza kupatikana kiasi cha sh.milioni 584.1 ikiwa 
fedha taslim milioni 113.4,ahadi milioni 471.6,mifuko ya saruji 400 na 
ndoo za rangi 50.
Akizungumza
 katika harambee hiyo iliyofanyika mjini Kibaha,Samia alieleza alisema 
ofisi yake inachangia milioni kumi na kudai ,jengo hilo lilisuasua kwa 
kipindi kirefu lakini chini ya usimamizi wake atasimamia ujenzi huo na 
hakuna fedha wala nondo zitakazopotea kama zilivyopotea wakati huo.
Alisema,
 CCM Pwani ina vitega uchumi ,lakini waache kubakia kuvihesabu kwa namba
 ,wasilale badala yake waviendeleze ili kupiga hatua kiuchumi na 
kuondokana na hali ya kuwa omba omba.
"Sisi
 sio masikini wa namna hiyo, tuliendekeza matumbo kuliko lililo mbele 
yetu, sasa tuache kuendekeza matumbo tufanye kazi,mkoa wa Pwani hauna 
sababu ya kupita kuombaomba, maana mna mtaji lakini pia mmelala"
"Tujipange vizuri, itabakia tunasema hiki chetu,kile chetu lakini hamviendelezi"alibainisha Samia.
Samia
 alifafanua, wahakikishe jengo hilo linakamilika mwezi June mwaka huu 
ili kuondokana na kupanga ukumbi wakati wa shughuli za chama.
Nae ,Jakaya Kikwete alishukuru na kufurahi kwa kualikwa kwenye shughuli hiyo,na atachangia mifuko 200 ya saruji.
Jakaya
 alisema ,wazo la ujenzi huo lina historia kwake, lilianza miaka mingi 
,":Nimefurahi sana kuona msukumo wa kuendeleza vitega uchumi hivi 
ambavyo vilisuasua lakini sasa vinaendelezwa kwa manufaa ya 
chama."alisema Jakaya.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo  ,aliwaomba ,wadau na wananchi kuendelea kuchangia ili kutimiza adhma hiyo.
"Tumepewa
 muda ,hadi mwezi June mwaka huu ,ujenzi uwe umekamilika hivyo juhudi za
 pamoja zinatakiwa ili tukamilishe kwa wakati huo"alifafanua Ndikilo.
Katika
 harambee hiyo, mfanyabiashara Bakhresa amechangia kiasi cha sh.milioni 
100,Shubash Patel anaezeka jengo zima kwa gharama ya milioni 250.
Mkuu
 wa mkoa wa Pwani Ndikilo alitoa sh.milioni 50,kamati ya siasa mkoa 
mifuko 200 ya saruji na sh.milioni nne,wabunge 13 wa mkoa huo 
wamechangia sh.milioni 16,ambapo rafiki wa mbunge wa viti maalum Zainab 
Vullu amechangia milioni 10.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...