Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema
Serikali imekusudia kumnyanga’anya shamba la mkonge la Kwashemshi
Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa
Tanga kwa kusababisha migogoro kwa wakazi wa eneo hilo na kukiuka
masharti ya uendelezaji.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo
pamoja na wamiliki wa shamba hilo la Kwashemshi Sisal Estate mara
baada ya kukagua miundombinu ya shamba hilo ambayo imeonekana
kuchakaa.
“kwanza umekiuka masharti ya uendelezaji, kwa sababu umepewa shamba
tangu mwaka 2003 na hadi leo ni miaka 17 hujalima lote wakati
ulitakiwa uwe umemaliza kulilima mwaka 2011. Pili tunakudai kodi ya
pango la ardhi hujalipa, tatu hujatoa ajira kwa wananchi na hujatoa
gawio kwa Halmashauri, sasa kwanini nisimshawishi Mhe. Rais afute hili
shamba?” amesema Mhe. Lukuvi.
Awali mkazi wa eneo hilo Bwana Musa Majaliwa amemlalamikia mwekezaji
huyo kwa madai ya kumiliki shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari
elfu tatu ambapo katika eneo lote ekari mia tatu pekee ndiyo zenye
mkonge na sehemu nyingine ni vichaka.
“tunachoomba Waziri Lukuvi utusaidia kupata sehemu ya ardhi hii kwa
matumizi ya kilimo na makazi kwa kuwa ongezeko la watu limekuwa ni
kubwa tofauti na hapo awali” alisema Bwana Musa.
Kwa mujibu wa Mhe. Waziri shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3,703
linamilikiwa na Ndugu Methew Upanga Mnkande maendelezo yake
hayaridhishi kwani hadi sasa eneo lenye mkonge wakuvuna (Mature) ni
ekari 1,210, eneo lenye mkonge mdogo (Immature) ni ekari 380 na
kufanya eneo lililoendelezwa kuwa na ukubwa wa ekari 1,590 sawa na
asilimia 42 tu.
Kuhusu kudaiwa kodi, mmiliki huyo tangu amilikishwe mwaka 2003 alikuwa
hajalipa kodi ya pango la ardhi na alikuwa anadaiwa shilingi 2//6yyyy
2,218,000 ambapo hadi sasa amelipa shilingi 8, 000,00 na deni hadi
sasa anadaiwa shilingi 14,218,000.
Kwa upande wake Mwakilishi wa mwekezaji wa shamba hilo ambae
anatambulika kwa jina la mzee Mkande amedai kuwa shamba hilo
limeendelezwa kwa kupanda mikonge mikubwa hekta mia nne thamani na
mkonge mdogo ambao unatajiwa kuvnwa hivi karibuni ni hekta 150.
Kuhusu madai ya kodi ya pango la ardhi wanazodaiwa na Serikali
mwakilishi huyo amekili kuwa awali walikuwa hawalipi kodi, ila sasa
wameingia makubaliano na wilaya kulipa ambapo mpaka sasa wameshalipa
kiasi cha shilingi milioni 8 na bado wanadaiwa kiasi cha shilingi
milioni 14 mpaka sasa.
Hata hivyo, Mhe. Lukuvi aliendelea kumbana mwakilishi huyo kwa
kumfahamisha kuwa shamba hili lipo kwenye hatua za ubatilishaji
kutokana na uvunjifu wa masharti ya kutoendeleza ipasavyo na kulipa
kodi ya ardhi kwa kusuasua.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wasimamizi wa shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga mbele ya wakazi wa eneo hilo. Kulia ni bwana John Mjengwa na katikati ni Mzee Mkande.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua miundombinu ya shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wasimamizi wa shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga mbele ya wakazi wa eneo hilo.
Baadhi ya miundombinu chakavu ya shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga.
Wakazi wa kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga
wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuvi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...