Mkurugenzi wa shirika la Ocode
Joseph Jackson wa kati kati akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya
ubungo Beatrice Dominic wa kushoto pamona na Afisa elimu wa manispaa
hiyo kulia wakiwa wameshikilia upete kwa ajili ya kuukata ikiwa ni
ishara ya uzinduzi wa darasa moja la wanafunzi wa elimu ya awali
Kibwegere ambalo limetolewa na shirika la Ocode kwa ajili ya kuboresha
sekta ya elimu.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma
katika shule ya msingi Kibwegere elimu ya awali wakiwa wameketi katika
madawati ambayo yametolewa kwa msaada wa shirika la Ocode katika halfa
ya makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo manispaa ya
ubungo Jijini Dar es Salaam/
Mkurugenzi wa Shirika la Ocode
Joseph Jackson akizungumza na baadi ya walimu, wanafunzi wa shule ya
msingi Kibwegere hawapo pichani wakati wa halfa ya makabidhiano ya
uzinduzi wa darasa jipya ambalo limejengwa kwa ajili ya wanafunzi wa
elimu ya awali kwa ajili ya kuwasaidia waweze kusoma katika mazingira
ambayo ni rafiki
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa
ya Ubungo Beatrice Dominic akifafanua jambo kwa walimu na wanafunzi
ambao walihudhulia katika halfa fupi ya makabidhiano ya chumba cha
darasa jipya ambacho kimejengwa kwa ajili ya kusomea watoto wa elimu ya
awali
Mkuu wa Shule ya Msingi Kibwegere
Charles Kulemba akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa halfa ya
uzinduzi huo wa darasa jipya mablo limejengwa mahusus kwa ajili ya
watoto wadogo wanaossoma katika ngazi ya awali
Mmoja wa walimu ambao
wanawafundisha wanafunzi wa elimu ya awali Bi. Eunice Matembo akisoma
Risala yake kwa mgeni rasmi amabye ni Mkurugenzi mteandaji wa Manispaa
ya Ubungo hayupo picha wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano ya madawati,
viti pamoja na uzinduzi rasmi wa darasa hilo la wanafunzi wa awali.
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya
Ubungo Beatrice Dominic wa katikati akijadiliana jambo na mwalimu mkuu
wa Shule hiyo ya Kibwegere pamoja na watumishi wengine wa Ocode na
serikali wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano wa misaada mbali mbali
ikiwemo meza pamoja na viti kwa ajili ya kukalia walimu.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya
Msingi Kibwegere wakiwa wanasikiliza hotuba ambayo ilikuwa inatolewa na
Mkurugenzi wa shirika la Ocode Joseph Jackson hayupo pichani wakati wa
sherehe ya uzinduzi wa darasa jipya ambalo limejengwa kwa ajili ajili
ya kuwasaidia watoto wa elimu ya awali.
Baadhi ya watendaji wa Shirika la
Ocode wakiwa wameketi kwa utulivu wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic hayupo pichani wakati wa halfa hiyo
ya uzinduzi wa darasa moja jipya lililojengwa kwa ajili ya wanafunzi wa
elimu ya awali.
Pichani ni kibao ambacho
kinaonyesha shule ya msingi Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya Ubungo
iliyopo Jijini Dar es Salaam.abpo shule hiyo imepatiwa msaada wa
madawati, 39 viti 13 vya walimu pamoja na kukabidhiwa darasa jipya kwa
ajili ya watoto wa elimu ya awali lililotolewa na shirika la Ocode na
kughalimu kiasi cha shilingi milioni 24(PICHA NA VICTOR MASANGU)
………………………………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, UBUNGO
SEKTA ya elimu
hapa nchini licha ya serikali ya awamu ya tano kuweka sera ya kutoa
elimu bure lakini bado katika baadhi ya maeneo ya shule za msingi na
Sekondari zilizopo katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam
zinakabiliwa na changamoto mbali mbali ya upungufu wa matundu ya vyoo
pamoja na uhaba na uchakavu wa miundombinu ya madarasa hivyo
kusababisha wanafunzi wengine kusoma katika mlundikano mkubwa.
Katika kuliona
hilo Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization Community
Development (OCODE) limeamua kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dk.
John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa msaada wa
madawati 39,ya wanafunzi, viti 13 vya kukalia walimu pamoja na kukabidhi
rasmi chumba cha darasa moja jipya kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya
awali katika shule ya msingi Kibwegere.
Akizungumzia
kuhusiana na msaada huo Mkurugenzi wa Shirika la Ocode Joseph Jackson
amesema kwamba kwa sasa wana tekeleza mradi wa elimu ambao utakuwa wa
kipindi cha miaka mitano ambao umeanza kufanyika tangu 2019- 2023 kwa
lengo la kuwez kuwasaidia watoto wa shule za awali na msingi katika
kuwawekea mazingira mazuri katika suala zima la upatikanaji wa kupata
elimu iliyo bora kwa manufaa yao ya baadae.
Aidha Mkurugenzi
huyo alibainisha kwamba katika mradi huo umeweza kugusa ujenzi wa
darasa hilo jipya la wanafunzi wa elimu ya awali ambalo mpaka kukamilika
kwake limegharimu kiasi cha shilingi milioni 26 na kwamba wana imani
kuwa watoto hao kwa sasa waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya kukaa
kwa mlindikano watasoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwao
“Shirika letu
la Ocode kwa sasa linaendelendea kutekeleza program ya mradi wa elimu
ambao utakuwa unazigusa baadhi ya shule za msingi ambazo zipo katika
maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es salaam, maana nia yetu ni
kuwasaidia watoto hawa kuanzia elimu ya awali na kwamba kwa sasa
tutajikita zaidi kwa wanafunzi wa daras ala kwanza na darasa la pili
pamoja na wale wanafunzi wa ngazi ya awali ili kuweza kuwajengea uwezo
wa kupata elimu bora,”alisema Mkurugenzi huyo.
Pia alibainisha
kwamba katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miaka
mitano watahakikishwa kwamba wanashirikiaa bega kwa began a serikali ya
awamu ya tano pamoja na wadau wengine wa maendeleo ili kuleta
mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia elimu kuanzia ngazi za chini na
kuendelea.
Kwa upande wake
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kibwegre akisoma risala kwa mgeni rasmi
katika halfa ya makabidhdiano ya madawati na uzinduzi wa darasa hilo
amebainisha kwamba kwa sasa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana
kutokna na ukosefu wa ofisi za walimu na vyumba vya madarasa ambapo
wakati mwingine inawalazimu walimu kufanyia kazi zao wakiwa wamekaa
chini ya miti hivyo msaada huo ambao umetolewa na Ocode utakuwa ni
mkombozi kwa upande wao.
“Shule yetu ya
Kibwegere kwa kweli tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa Shirika
ili la Ocode kwani wameweza kutuona na kutusaidia katika mambo mbali
mbali ya kutujengea darasa moja, kutupa viti, pamoja na madawati ya
wanafunzi hii kwa upande wetu ni moja ya hatua, kwani hapo awali hali
ilikuwa ni ngumu kutokana na miundombinu yenyewe ya madarasa pamoja na
ofisi za walimu, hivyo napenda kushukuru sana,”alisema Kulemba.
Kwa upande wake
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya makabidhiano amesema kwamba pamoja
na juhuzi zinazofanywa na serikali lakini amekiri bado kunachanagmoto
kubwa ya miundombinu ya madarasa kwa shule ya msingi na sekondari na
anatambua walimu wanafanya kazi zao katika mazingira magumu sana hivyo
amelipongeza shirika la Ocode kwa kuamua kushirikiana na serikali katika
kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi ya awali.
SHULE ya msingi
Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya Ubungo nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 1741 ambao wanakabiliwa na
changamoto mbali mbali ikiwemo upungufu wa walimu, uhaba wa miundombinu
ya madarasa, ofisi za walimu, pamoja na matundu ya vyoo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...