Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (katikati), akizungumza na Kaimu Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Victor
Mwambalaswa wakati wakitoka kukagua Jengo la Makao makuu ya Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. Kamati ya Bunge imeridhishwa na ujenzi
wa Jengo hilo ambalo lipo hatua ya mwisho kukamilika.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama (hawapo pichani), katika kikao cha Kamati hiyo, kilichofanyika
Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma, leo. Kamti
hiyo pia ilikagua ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Jeshi hilo na
imeridhishwa na ujenzi wa Jengo hilo ambalo lipo hatua ya mwisho
kukamilika. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima, na kulia ni
Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Masunga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,
Almas Maige, wakiliangalia Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji wakati Kamati hiyo inafanya ukaguzi wa jengo hilo ambalo lipo
hatua ya mwisho kukamilika. Kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi wa jengo
hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene, akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, uimara wa kuta za jengo la Makao
Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma, wakati wajumbe hao walipokuwa wanalikagua jengo hilo ambalo lipo hatua ya mwisho kukamilika. Kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi wa jengo hilo. Wapili kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Victor Mwambalaswa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (watatu kushoto-waliokaa), Kaimu Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Victor
Mwambalaswa (katikati-waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Ramadhani Kailima (wapili kushoto-waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga (kulia waliokaa), wakiwa katika
picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo, baada ya kumaliza kufanya
kikao na baadaye kulikagua Jengo la Jeshi hilo, jijini Dodoma, leo.
Muonekano wa Jengo la Makao Makuu
ya Jeshi la Zimamoto na Uoakoji, jijini Dodoma, lipo hatua ya mwisho
kukamilika, ambapo wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama walilikagua na kuridhishwa na ubora wa Jengo hilo.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...