Kampuni ya Star Media(T) kupitia chapa yake StarTimes imeunga mkono jitihada za Serikali kupambana na kuelimisha jamii kuhusiana na virusi vya COVID-19, StarTimes imeanza kurusha kipindi cha StarTimes Daily Covid-19 Report kinachotoa habari/ taarifa kuhusu virusi vya Corona na Elimu ya namna ya kujikinga ,kupitia chaneli ya ST Swahili kila siku saa 3:45 usiku,na pia kupitia Application ya StarTimes ON kwenye simu janja.
Lengo ikiwa ni kuwahabarisha watu wa mijini na vijijini na kuwaelimisha namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Covid -19, watu wamekua na wasiwasi mkubwa na maswali mengi kwa kupata habari zisizo sahihi kupitia mitandao ya kijamii,hii imepelekea kua na ugumu wa upatikanaji wa habari za uhakika,hivyo basi StarTimes itawahabarisha na kuwaelimisha kuhusiana na virusi vya Covid -19.
Zingatia Tahadhari zitolewazo na mamlaka husika,Jihadhari na uwalinde wengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...