Meneja Mafunzo kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Dickson Mwanyika akizungumza na Michuzi Tv baada ya kumalizika mkutano kwa Njia ya Mtandao uliohusisha nchi mbalimbali kuhusu Virusi vya Corona leo jijini Dar es Salaam,ambapo amempongeza Rais Magufuli kwa kusitisha mbio za Mwenge mwaka huu mpaka pale hali ya tatizo la Virusi vya Corona litakapopatiwa ufumbuzi huku bajeti ya Mwenge akiagiza iende Wizara ya Afya kununua Vifaa na dawa za Corona.
Dkt.Kija Luhuti
(kushoto) akizungumza na Michuzi Tv
baada ya kumalizika mkutano kwa Njia ya Mtandao uliohusisha
nchimbalimbali kuhusu Virusi vya Corona leo jijini Dar es Salaam. ambapo amesema wananchi wazingatie
usafi ili kujikinga
na Virusi vya Corona kulia ni Meneja Mafunzo toka Wakala wa Mafunzo
kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Dickson Mwanyika
Watumishi Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) pamoja na wadau mbalimbali wawakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video (Tele Conference) leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Tanzania TaGLA,Fredrick Massawe akiwashukuru wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano kwa Njia ya Mtandao uliohusisha nchi mbalimbali kuhusu Virusi vya Corona leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...