Meneja wa Bidhaa za Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Muyonga,akiongea katika uzinduzi wa simu aina Samsung S20,pembeni yake ni Meneja wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohamed.
Wateja watakaonunua simu hiyo watajipatia Gb78 za intaneti kwa mwaka mzima
Dar es Salaam. Machi 13, 2020. Kampuni inayoongza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo kwa kushirikiana na Samsung Electronics wamezindua Simu janja aina ya Samsung S20 nchini Tanzania.Simu hizo tatu ni Galaxy S20, Galaxy S20+ na Galaxy S20 Ultra.
Ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kuongea matumizi ya mtandao wa 4G na kuchangia ukuaji wa teknolojia ya kidigitali nchini.
Meneja wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Muyonga akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo alisema “Ni jambo la kubwa sana kwetu kuchaguliwa na Samsung kuwa wa kwanza kuzihifadhi na kuuza simu za Samsung S20 kwenye soko la Tanzania.Hii inaonesha imani yao kwetu juu ya chaneli kubwa za usambazaji tulizonazo na pia kupitia timu yetu ya huduma kwa wateja inayotoa huduma zenye ubora wa hali ya juu,”alisema Muyonga.
“Lengo letu ni kuchochea mageuzi ya kidigitali katika maisha ya watu hapa nchini na ndio maana tumeungana na Samsung ili kuongeza idadi ya umiliki wa simu janja pamoja na matumizi ya data ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanaifikiwa na teknolojia hii,” alisema Muyonga.
Muyonga aliongeza “Tunalenga kuongeza ueneaji wa simu janja nchini huku tukihakikisha wateja wetu wanafurahia huduma za kidigitali kupitia mtandao mkubwa wa 4G hapa nchini.Na ndio maana tunatoa 78 Gb za intaneti kwa mwaka mzima kwa wateja wote watakaonununa Samsung S20,” alisema .
Akizungumza wakati wa uzindizu huo, Meneja wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohamed alisema Samsung imezindua simu ya Samsung Galaxy S20 toleo jipya ulimwenguni ambayo itabadilisha namna ambavyo watu wanavyoishi na kuufurahia ulimwengu.
Galaxy S20 ina camera ambayo ina uwezo wa kipekee wa kupiga picha huku ikiwa na sifa mbalimbali ambazo zitamfanya mtumiaji kufurahia kuitumia ikiwamo muziki,video zenye ubora pamoja na michezo (games) mbalimbali.
“Tukiwa tunaingia kwenye muongo mwingine, kuna mabadiliko makubwa kwenye sekta ya mawasiliano na namna watu wanavyo ujua na kuufurahia ulimwengu.Samsung inahakikisha inatoa teknolojia na vifaa vya kisasa zaidi ili kuendana na mabadiliko hayo.Kwa kutumia camera yenye mfumo wa AI unaweza kupata kila tukio na kuungana na uwapendao bila mipaka,” alisema Mohamed.
Simu ya Galaxy S20 itauzwa kwa Sh2,235,000, na S20+ kwa Sh2,480,000 huku S20 Ultra kwa sh 3,100,000.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...