Inafahamika wazi namna gani teknolojia imesaidia nchi nyingi kuendelea kiuchumi. Hii inadhihirika wazi pia kwa nchi za Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo matumizi ya simu za mkononi na mtandao wa intaneti vimesaidia kukuza fursa nyingi za biashara na mamilioni ya watu. Sasa teknolojia ndiyo inaendesha biashara, kuanzia kuagiza malighafi hadi kupokea malipo toka kwa wateja.

Katika eneo la kilimo nako teknolojia inabadilisha mambo kuwa bora zaidi. Wakulima katika nchi za Ethiopia, Kenya na Rwanda sasa wanapata taarifa za soko la mazao, hali ya hewa na hata nini cha kupanda kwenye udongo wa namna gani, kupitia simu zao za mkononi. Mabadiliko haya yanaongeza tija kwenye kilimo na kwa ujumla yanabadili maisha ya watu. 

Hata hivyo, maendeleo kama haya ili yawe na faida zaidi siku zijazo yanahitaji wananchi kuwa na elimu ya kidijitali. Takwimu za Benki ya Dunia zinaoneyesha nafasi za kazi milioni 230 katika eneo la Ukanda wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara zitahitaji watu wenye ujuzi wa kidijitali (digital literacy) kufikia mwaka 2030, hii ni miaka 10 tu toka sasa. Ujuzi huo ni ule wa msingi kama mawasiliano ya barua pepe, kufanya tafiti kwa kutumia mtandao, malipo mtandaoni, kutunza data na kutumia programu za kompyuta. 

Kuhakikisha kwamba Tanzania inavuna faida za maendeleo ya teknolojia ya kidijitali lazima kuwekeza katika watoto na kuhakikisha wanapata elimu ya kidijitali na kukuza ujuzi wao. Kwa bahati nzuri, kampuni za simu Tanzania katika miaka ya karibuni imefanya kazi kuwekeza katika wanafunzi ili kukuza ubora wa nguvu kazi ya kizazi kijacho. Mfano wa kampuni mojawapo ni Tigo Tanzania ambayo mwaka jana ilizindua kampeni ya kuelimisha wanafunzi wa kike ujuzi wa namna mbalimbali kama uandishi wa programu za kompyuta (coding) na uchambuzi wa taarifa. Mipango kama hii ni muhimu kumuinua mtoto wa kike na kuandaa nguvu kazi sahihi kwa kizazi hiki. 

Lazima lakini kukumbuka kwamba mpango kama huu wa Tigo umewezekana kutokana na uwekezaji wa muda mrefu pamoja na kampuni nyingine. Uwekezaji zaidi wa namna hiyo utahakikisha kampuni hizi za simu zinafanya zaidi kukuza ujuzi wa kidijitali kwa Watanzania.
Tuendelee kufurahia matunda haya ya sekta ya mawasiliano na teknolojia yanayotokana na uwekezaji na ubunifu wa makampuni ya simu, kwa kuhakikisha tunajenga mazingira bora zaidi ya uwekezaji na uendeshaji biashara ili tuvune matunda zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...