TAKWIMU zinaonyesha kwamba Tanzania imepitia kipindi kizuri cha ukuaji wa kiuchumi katika muongo mmoja uliopita na kuifanya hivi sasa kuwa moja ya chumi zinazokua vizuri katika eneo la Afrika Mashariki.
Ripoti ya UK ThinkTank inaongeza kuwa mafanikio ya ukuaji wa kiuchumi Tanzania yamewezeshwa na juhudi za serikali kukuza sekta ya viwanda na kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Matokeo ya juhudu hizo yameifanya Tanzania kuwa mmoja ya wauzaji wakubwa nje wa dhahabu na pia kuwa moja ya nchi inayopata watalii wengi zaidi barani Afrika.
Wakati huo huo serikali ya Tanzania imeendelea kujiweka imara katika kuwekeza kwenye miundombinu muhimu kama miradi ya Standard Gauge Railway (SGR), kupanua zaidi bandari na kuunganisha maeneo ya vijiji na nishati ya umeme.
Ripoti hiyo ya UK ThinkTank inaeleza kuwa maendeleo ya Tanzania yamechangiwa sana na ubunifu katika teknolojia na uwepo wa huduma nzuri ya mawasiliano ya simu na data. Maendeleo haya katika teknolojia ni matokeo ya uwekezaji wa muda mrefu kwenye sekta ya mawasiliano ya simu ambayo taarifa zinaonyesha kuwa mpaka sasa ni uwekezaji unaozidi shilingi za Kitanzania trilioni 6.
Uwekezaji huu katika sekta ya mawasiliani ya simu za mkononi umekuza sana mabadiliko ya kidijitali Tanzania mfano huduma ya kasi ya 4G na mtandao wa intaneti kupitia simu za mkononi. Ubunifu katika sekta hii pia umeleta huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambapo zaidi ya watu milioni 25 Tanzania sasa wanatumia simu zao kutuma, kupokea, kulipia huduma na hata kutunza fedha.
Wafanyabishara wadogo na wa kati nao wanafurahia maendeleo ya sekta ya mawasiliano ya simu ambayo inawasaidia kuendesha biashara zao kwa namna mbalimbali kama kuwapa intaneti, kupokea malipo, kulipia huduma mbalimbali, kutangaza bidhaa mitandaoni na hivyo kupunguza gharama za kuendesha biashara, miaka si mingi nyuma ilikuwa lazima ukapange foleni benki kufanya huduma nyingi ambazo leo unazifanya kupitia simu yako.
Uimara wa sekta hii ya mawasiliano ya simu ni jambo muhimu na ili uendelee ni budi kuendelea kujenga mazingira bora ya sekta hii kukua. Kujenga mazingira ya sekta binafsi kuwekeza mtaji zaidi huku serikali ikiendelea kuweka sera bora za kuratibu sekta hii ni mambo muhimu kuwezesha sekta kukua zaidi ili Tanzania na Watanzania wote wazidi kunufaika zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...