Na Karama Kenyunko,Michuzi Globu.
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara, Abdul Nsembo maarufu kama Abdulkandida (45) na mkewe, Shamim Mwasha(41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Pia upande huo wa mashitaka umeiomba mahakama kuipanga kesi hiyo katika tarehe ya karibu ili waweze kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya mashahidi (Commital) na vielelezo kwa ajili ya kesi hiyo kuhamia Mahakama Kuu ambayo ndio ina mamlaka ya kuisikiliza.
Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai hayo leo Machi 27, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashidi Chaungu wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa
Baada ya maelezo hayo Hakimu Chaungu aliahirisha shauri hilo hadi Aprili Mosi mwaka kwa ajili ya washitakiwa hao kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo na kisha kwenda Mahakama Kuu.
Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog ya 8020 Fashion na mumewe wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019, wakidaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70
Washitakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 13, mwaka jana.
Katika hati ya mashtaka inadaiwa Mei Mosi, mwaka jana huko Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, washitakiwa walisafirisha dawa hizo huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...