Charles James, Globu ya Jamii

WANAFUNZI wa Vyuo Vikuu na vya kati jijini Dodoma wameishukuru serikali kwa kufunga vyuo hivyo ili kuondoa msongamano katika maeneo yao ya vyuo unaoweza kusababisha maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.

Wakizungumza na Michuzi leo jijini Dodoma wanafunzi hao wamesema kuwa ikitokea mmoja wao amekumbwa na virusi vya corona ingeweza  kusambaa kwa kasi kubwa na kupelekea maambukizi kuenea kwa haraka zaidi hivyo serikali imefanya jambo la busara kufunga vyuo na shule za awali hadi Sekondari kwa simu 30.

Wanavyuo hao  wamelalamikia adha ya usafiri wanayokumbana nayo hasa kwa wale wanaoenda mikoani ambapo magari yamekua machache kulinganisha na idadi ya wasafiri lakini pia nauli ikipandishwa kulingana na kiwango cha kawaida.

‘’ Kiukweli usafiri umekua changamoto sana kwetu unafika unakuta tiketi hazipo unashangaa magari yameisha ,unaambiwa kama unataka kuondoka ndani ya huo muda uongeze hela sasa kwa sisi tunaokaa mikoa ya mbali tunaangaika kwa kweli.

Mfano mimi kwetu ni Mkoa wa Mara nauli ya kwenda kwetu ilikua Sh 40,000 lakini sasa imepanda hadi 47,000 na wengine wanachaji hadi 50,000 jambo hili linatuwia vigumu sana na ndio maana toka jana tupo hapa," Amesema mmoja wa wanafunzi hao.

Ikumbukwe serikali imezifunga shule zote za kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita pamoja na vyuo vyote vikuu na vile vya kati kwa siku 30 hadi pale ambapo Wizara ya Afya itakavyotoa utaratibu.

 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM wakisubiri usafiri kwa ajili ya kuelekea makwao baada ya Serikali kuvifunga vyuo vyote nchini pamoja na shule za msingi na sekondari kwa ajili ya kuepuka maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vilivyopo jijini Dodoma wakiwa kituoni kusubiri magari kwa ajili ya kuelekea majumbani mwao baada ya serikali kuvifunga vyuo vyote kwa ajili ya kuzuia msongamano unaoweza kusababisha maambukizi ya virusi vya Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...