Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa Kongamano
la Biashara na Uwekezaji kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na
Wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki
katika Ukumbi wa Mikutano Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12
Machi, 2020
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas
Ndumbaro wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Jumuiya
ya Nchi za Afrika Mashariki na Wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara wa
Uswidi na Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano Serena Hotel
Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2020
Rais wa TCCIA Bw.
Paul Koyi akihutubia wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati
ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na Wanachama wa Chemba ya
Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano
Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2020
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Swiden Mhe. Dkt. Wilibrod Slaa wakati wa kongamano hilo.
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mada mbalimbali katika Kongamano hilo.
Sehemu ya wajumbe
wakifuatilia mada mbalimbali katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji
kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na Wanachama wa Chemba ya
Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano
Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2020.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF, Godfrey Sembeye
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Kipindi cha Supa
Breakfast kinachorushwa na Eastafrica radio wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiteta jambo na
Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt. Wilibrod Slaa wakati wa
Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika
Mashariki na Wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika
Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano Serena Hotel Jijini Dar es Salaam
tarehe 12 Machi, 2020
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki pamoja na meza
kuu wakifuatilia hoja wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati
ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na Wanachama wa Chemba ya
Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano
Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2020
Mwenyekiti
wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki Bw. Jan
Furuvald akiwasilisha mada wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Zungu akieleza mikakati ya ofisi yake katika kuvutia wawekezaji wakati wa Kongamano
la Biashara na Uwekezaji kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na
Wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki
katika Ukumbi wa Mikutano Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12
Machi, 2020.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
*********************************
MWANDISHI WETU
Serikali kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu imewezesha kuanzisha mfuko maalum wa kukopesha watu
wenye nia ya kuwekeza kwenye viwanda vya kati na vikubwa lengo likiwa
ni kuwanufaisha Watanzania waliokosa mitaji na wenye nia ya kuwekeza
nchini.
Mfuko huo
ulioanzishwa Februari 22 mwaka huu utakuwa ukikopesha Watanzania kuanzia
kiwango cha shilingi milioni 8 hadi 50 kwa wenye nia ya kuwekeza
viwanda vya kati na shilingi milioni 50 hadi 300 kwa wenye nia ya
kuwekeza kwenye viwanda vikubwa.
Aidha, ofisi hiyo
inashirikiana na taasisi nyingine kuendesha mfuko huo ikiwepo Mfuko wa
Hifadhi za Jamii (NSSF), Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC), Shirika la Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO) na Mamlaka ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Hayo
yamebainishwa hii leo (Machi 12, 2020) Jijini Dar Es Salaam na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah
Kairuki wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya
kufungua Kongamano la pili la Biashara na Uwekezaji la Nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sweden linaloendelea kwa siku mbili
Jijini humo.
Kairuki amesema
Tanzania hivi sasa imeimarisha Mazingira ya Uwekezaji ambapo tangu
kuingia kwa Rais Magufuli Madarakani hakuna kodi yoyote iliyoongezwa
kwenye biashara na uwekezaji huku kodi zaidi ya 168 zikifutwa katika
kipindi cha miaka miwili zikiwepo kodi 105 za kilimo.
Wakati akifungua
Kongamano hilo Waziri Kairuki aliwataka Wawekezaji wa ndani na nje ya
nchi kuwekeza nchini Tanzania kwa kueleza kuwa Sera, Sheria na
miundombinu yake imeboreshwa kwa kiwango kikubwa.
“Tunazo fursa
nyingi za uwekezaji hapa Tanzania, tuna fursa kwenye Kilimo cha mazao ya
chakula na biashara pamoja na mnyororo wake wa thamani kwenye sekta
hiyo, tunahitaji uwekezaji wa viwanda mbalimbali vikiwepo vya Dawa na
vifaa tiba, mafuta ya kula na vinginevyo vingi” alisema Waziri Kairuki.
Kwa upande wake,
Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt Wilbrod Slaa amesema
Wafanyabiashara wa NORDIC wameisifu Serikali ya Tanzania kwa kuondoa
rushwa na kuimarisha utendaji wa wazi Serikalini suala ambalo awali
lilikuwa likuwapa changamoto kubwa.
“Nimekuwa
nakutana na wafanyabiashara na wawekezaji wengi wa Sweden jambo kubwa
nililolipata kutoka kwao ni kwamba wanashukuru tangu Serikali ya Awamu
ya Tano ilivyoingia madarakani mambo ya chini ya meza hayapo tena,
angalau sasa wanafanya biashara juu ya meza wengine walifikia hatua ya
kufunga biashara zao, lakini pia naomba nishauri tu vibali vya
wawekezaji viharakishwe ili kwenda na wakati”, alisema Dkt. Slaa.
Kongamano hilo
ambalo kwa mara ya kwanza lilifanyika Stockhom Sweden mwaka 2012
lilikuja ma naadhimio kadhaa ya kushirikiana katika kuimarisha uchumi wa
nchi hizo kibiashara na uwekezaji lilileta matokeo chanya kufuatia
kuwepo kwa wawekezaji wengi wa Sweden kuwekeza kwenye nchi za Afrika
Mashariki.
Mkutano huo
umehudhuriwa na zaidi ya makampuni makubwa 20 toka Sweden kupitia Chama
chao cha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Afrika Mashariki (SWEACC)
ambapo Mwenyekiti wake Bw. Jan Furuvald amesema uwekezaji kwenye nchi
hizo umekuwa na manufaa kutokana na kuwa na soko kubwa la watumiaji wa
bidhaa zao na kuwataka wawekezaji wengine kutoka nchini kwake kuja
kuwekeza Afrika Mashariki.
“Sisi
Wafanyabiashara na wawekezaji mara nyingi tunaangalia mazingira mazuri
ya uwekezaji, kuwekeza kwenye nchi za Afrika Mashariki kunatuhakikishia
soko kubwa kwani licha ya kuwa kwenye jumuiya hii pia kuna fursa
nyingine za SADC”, alisema Furuvald.
Kongamano hilo
lenye kauli mbiu ya “Green Solutions in East African Cities” Suluhisho
la Kijani kwenye Majiji ya Afrika Mashariki linalenga kuimarisha
mazingira ya uwekezaji kwenye majiji yaliyopo kwenye Jumuiya hiyo ambapo
kwa Tanzania, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, Mhe. Mussa Zungu amesema ili kukabiliana na hali hiyo hatua
kadhaa zimechukuliwa.
Alizitaja hatua
hizo kuwa ni pamoja na kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki
ambayo ilikuwa ikichafua mazingira na kuharibu mazalia ya viumbe hai
ambapo pia kwa sasa Serikali inahamasisha matumizi ya gesi viwandani,
majumbani na kwenye magari ili kuepukana na uchafuzi wa mazingira na
ukataji miti hivyo kwa ajili ya matumizi ya nishati za mkaa na kuni.
Waziri Zungu
amesema katika kuhakikisha nishati mbadala inapatikana kwa urahisi
Serikali inajenga Bwawa kubwa la kufua umeme la Nyerere ili kuwe na
umeme wa uhakika.
Aidha Zungu
aliwataka wawekezaji wote waliokwama kupata vibali vya mazingira
kutokana na mazingira ya rushwa kufika ofisini kwake kwa ajili ya kupata
vibali hiyo.
“Kwa Wawekezaji
waliokwama kupata vibali vya mazingira wanione, tutawapatia vibali vyao
bila kuhangaika, hakuna jambo baya Duniani kama kumnyima mtu haki yake
ili upate pesa, tunathamini wawekezaji na tunathamini uwekezaji katika
nchi yetu” alisema Zungu.
Naye, Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya akasema
Serikali ya Tanzania imekuwa ikiweka mazingira mazuri ya biashara kwa
kuimarisha miundombinu Sera na miundombinu ambapo kwa sasa ujenzi mkubwa
wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge unaendelea lengo likiwa ni
kuzifanya nchi hizo kunufaika kwa usafirishaji kauli inayoungwa mkono na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Damas Ndumbaro.
“Kazi ya Serikali
yetu ni kuweka mazingira mazuri ya Biashara na Uwekezaji yakiwepo ya
Sera, Sheria na Miundombinu, kuimarisha Blue print na hali ya kisiasa
ambayo ina tija kubwa kiuchumi”, alisema Mhandisi Manyanya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...