Waziriwa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akipata maelezo ya namna ya shughuli yaujenziwa mradi wa jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania(TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni yaPetra Constuction co. Limited, NicholausMlayi alipotembelea mradi huo Kunduchi Dar es Salaam.
Waziriwa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akipata ufafanuzi kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya Y&P Architect inayosimamia Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam, Anna Shayo alipotembelea mradihuo Kunduchi Dar es Salaam. Waziriwa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiangalia ramani ya mradi wa jengo la Maabara ya Taasisiya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam baada ya kutembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo na kuunda tume kuchunguza mradi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI, Dk. Ismael Kimerei .
WAZIRIwa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesimamisha malipo yote kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Petra Construction co. Limited inayojenga maabara ya kisasa ya
Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaam hadi uhakiki wa gharama
halisi za mradi huo utakapokamilika baada ya kubaini kuwepo matumizi mabaya ya
fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 2.6
HivyoWaziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo.
Akizungumzamara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) jijini Dar es Salaam, WaziriMpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogoikilinganishwa na mkataba ulioridhiwa wash. bilioni 2.6 na kwamba taarifa ya uhakiki ya mradi huo itawasilishwawizarani ikiwa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya wizi huo wa fedhaza umma.
WaziriMpina alisema thamani halisi ya mradi huo hailingani na fedha zilizotolewa na
Serikali huku akitolea mfano baadhi ya miradi ya ujenzi wa majengo mbalimbali
ikiwemo vituo vya afya na hospitali za wilaya zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.
Hatahivyo wakati wa mjadala ukiendelea wa kuhoji matumizi ya fedha hizo kwenye
mradi huo, mmoja wa wakandarasi wanaojenga majengo hayo alimweleza Waziri Mpina
kuwa hadi mradi utakapomika kutabaki ‘chenji’ kiasi cha shilingi milioni 500
jambo lililotilia mashaka na kuibua maswali mengi juu ya gharama halisi za
mradi huo.
Kufuatia mkanganyiko huo wa maelezo yamkandarasi na hali halisi iliyoonekana kwenye mradi huo ndipo Waziri Mpinaakalazimika kutangaza uamuzi huo wa kuundwa tume hiyo ili iweze kufanya tathminiya gharama ya mradi iliyofanywa na Mshauri mwelezi wa mradi, namna zabuni ya
kumpata mkandarasi ilivyotangazwa na namna mshauri mwelekezi alivyopatikana na
hali ya ujenzi unavyoendelea kwa sasa ili kujua dosari ilisababishwa na nani.
Hivyo Waziri Mpina akabainisha kuwa baada ya kazi hiyo ya uhakiki kukamilika ndani ya siku saba ukweli utajulikana na hatua zote zilizopitiwa katika mradi huo ili kubaini kama Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 ilikiukwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha za umma.
“Sikubaliani na hizi gharama za mradi majengona miundombinu ni midogo ikilinganishwa na mkataba wa bilioni 2.6, BOQilihakikiwa na wahandisi wa wizara, washauri waelekezi walijiridhisha kwambaiko sawa na ujenzi ukaenda hadi bilioni 2.6 mtu yeyote akija anakataa” alihoji
Waziri Mpina.
HivyoWaziri Mpina ameagiza ujenzi wa mradi huo uendelee bila kusimama na ukamilike ifikapo Aprili 20 mwaka huu kama mkataba unavyoeleeza na baada ya jengo litazinduliwa ikiwa ni sehemu ya kuleta mageuzi makubwa ya sekta ya uvuvi kupitia eneo hilo muhimu la utafiti.
“Nitaletatimu ya ukaguzi itakayofanya uhakiki wa thamani ya fedha katika ujenzi wa jengo hili, kuanzia kwenye kutangaza tenda yenyewe, thamani ya mradi, kumpata
mkandarasi mwenyewe, cost estimates zilizofanywa na wizara na baadae watafanya
uhakiki wa kinachoendelea kujengwa hapa na kujua thamani halisi inayotakiwa na
kwanini mradi huu upitishwe hadi kusainiwa”alihoji Waziri Mpina.
Menejawa Mradi wa Swiofish, Flora Luhanga alisema mradi huo wa ujenzi wa Jengo la
Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ulianza Juni 10, 2019 kwa gharama ya
shilingi bilioni 2, 609,491,754 unajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Petra
Construction Limited na kusimamiwa na Kampuni ya YP Architect.
Luhangaalisema mradi huo unajumuisha pia ujenzi
wa uzio, ofisi ya walinzi, kuchimba kisima cha maji, ujenzi wa tenki la maji ya
mvua na kujenga mnara wa maji.
Mkandarasiwa Mradi huo, Nicholaus Mlayi alisema hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 70 na tayari ameshalipwa shilingi milioni 963 na unatarajia kukamilika
mwezi Aprili.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Uvuvi, Magese Bulayi alimhakikishia Waziri Mpina kuwa maagizo yote aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu hasa katika kuangalia thamani ya fedha ‘value for money’ katika mradi huo na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa
wote watakaobainika kuhusika katika mchakato huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...