Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na
Watendaji Wakuu wa Jeshi na Polisi Zanzibar, katika ukumbi wa mikutano
wa Jeshi hilo, Mjini Unguja, leo. Simbachawene amesema atafuatilia kwa
viongozi baada ya kupokea taarifa ya Jeshi lake, kuwa mtuhumiwa wa dawa
za kulevya mjini humo kuachiwa huru na mahakama kwasasabu ya kukosekana
kwa mkalimani. Pia alishangazwa na baadhi watuhumiwa wa dawa za kulevya
kuachiliwa huru na mahakama kwa kupewa adhabu ndogo ambacho hakiendani
na ukubwa wa kosa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akisalimana na
wananchi walinaosubiri kuhudumiwa na Maafisa Uhamiaji Makao Makuu,
Zanzibar, leo, wakati alipokuwa anawasili katika ofisi hizo kwa ajili ya
kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Uhamiaji. Pia, Waziri huyo alikutana
na Viongozi wa Polisi na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika ziara
yake ya siku moja mjini humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia)
akimsikiliza Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya
Zanzibar, Khadija Kheir Othman, wakati alipokuwa anafanya ziara katika
ofisi hizo, leo. Waziri huyo aliwataka maafisa hao kufanya kazi kwa
uadilifu pamoja na kushirikiana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati meza
kuu) Mkuu wa Sheria Uhamiaji Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Idara hiyo,
Hosea Kagimbo, wakati alipokuwa anazungumza na Watendaji Wakuu wa Idara
hiyo, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na
Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, katika kikao
kilichofanyika ukumbi wa mkutano wa Idara hiyo, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, alipomtembelea ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...