Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara iliwasilisha katika kikao hicho Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21. Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salim Mwinyi Rehani, na kulia ni Katibu wa Kamati hiyo, Ramadhani Abdalla. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Hasna Mwilima, nje ya Ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akijipaka kitakasa mikono (Sanitizer) nje ya Ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma, leo, kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (kulia), na Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wanja Mtawazo, wakipanga nyaraka kwa ajili ya kuziwasilisha katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara iliwasilisha katika kikao hicho Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...