Na. Catherine Sungura-Zanzibar

Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Hamad Rashid Hamad ameushukuru ujumbe wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania bara kutuma wataalam wake kutoka sekta mbali mbali zinazoshirikiana katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Corona.

Mhe. Hamad ameyasema hayo leo ofisini kwake Zanzibar wakati akiongea na timu ya wataalam kutoka Tanzania bara waliofika visiwani hapa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo.

“Tunapaswa kudhibiti ugonjwa wa corona  hapa nchini  hivyo bila ya kushirikiana  katika kuzuia na kukabiliana ugonjwa huu kwa wananchi wetu haitofaa,kukaa pamoja na kushirikiana itatusaidia kuwaelimisha wananchi hata  kuwaepusha”.Alisema Mhe. Hamad.

Aidha, waziri huyo alisema wizara ya afya ni kwa maisha ya wananchi hivyo inapaswa pande zote mbili kuimarisha umoja na muungano ili kuweza kuzuia na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na ugonjwa wa corona na magonjwa mengine ya mlipuko.

“Tumefanya uelimishaji kwa makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, tunashukuru viongozi hao wameitia vyema na hivyo wanatusaidia kutoa elimu kwa waumini wao ikiwemo kujua dalili na jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa corona”.

Naye Mganga Mkuu wa Serikali kutoka wizara ya afya Tanzania bara Prof. Muhammad Bakari Kambi amesema kuwa mashirikiano baina ya serikali hizi mbili ni muhimu sana ili kuweza kusaidiana katika vita ya kudhibiti ugonjwa huo na kujiweka tayari kuukabili.

Hata hivyo Prof. Bakari ameipongeza serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa utayari katika maeneo yote hatarishi ambayo timu hiyo ya wataalam iliweza kutembelea ikiwemo uwanja wa ndege,bandari na sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya matibabu.

Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima  ameipongeza Zanzibar kwa maandalizi ya  utayari wa kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na virus vya corona na hivyo kama serikali za mitaa wamejifunza mengi na hivyo itawasaidia wao katika kuboresha maeneo mengine ili kuweza kuzuia ugonjwa huo .

Ujumbe wa wataalam mbalimbali kutoka Tanzania bara wapo Zanzibar   kwa ajili ya kubadilishana uzoefu  pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabliliana na ugonjwa wa corona na kuona  utayari wa kudhibiti.

Timu hiyo imewajumuisha wataalam kutoka wizara ya afya,TAMISEMI, Mambo ya nje pamoja na ofisi ya waziri mkuu-maafa na wameweza kutembelea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid karume,hospitali ya mnazi mmoja,bandarini pamoja na eneo maalumu la matibabu lililopo Kidimni wilaya ya kati-unguja.
Ujumbe kutika tanzania bara pamoja na wataalam wa serikali ya mapinduzi zanzibar wakiangalia eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya matibabu lililopo Kidimni wilaya ya kati.
Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ) Mhe. Hamad Rashid Hamad akiongea na ujumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-bara waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Waziri Hamadi Rashid Hamad wakiagana.na Mganga Mkuu wa Serikali-Tanzania Bara Prof. Muhammad Bakari Kambi.
Waziri wa Afya-SMZ akiagana na Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Dkt. Doroth y Gwajima mara baada ya kufanya kikao cha mashirikiano cha kukabiliana na Corona.
Ujumbe kutoka tanzania bara wakiangalia eneo maalum lililopo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Karume litakalotumika kupumzisha muhisiwa wa corona endapo atatokea.
Muonekano wa eneo maalumu(Isolation Center) lililopo uwanja wa ndege wa kimataifa visiwani Unguja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...