Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiangalia chupa za
plastiki zilizo katika mchakato wa kurejelezwa alipotembelea kiwanda cha
A One Products & Bottlers Recycle Unit cha Mbagala jijini Dar
es Salaam alipofanya ziara ya kukagua na kuwakumbusha wajibu wao katika
ukusanyaji na kuwasogezea karibu wanachi wanaokusanya chupa hizo ikiwa
ni sehemu mojawapo ya kuhifadhi mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa maelekezo
mbalimbali alipotembelea kiwanda cha cha A One Products &
Bottlers Recycle Unit cha Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo aliahidi
Serikali kushirikiana nao huku akiwakumbusha wajibu wao katika utunzaji
wa mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongozana na
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua
kiwanda cha kurejeleza chupa cha plastiki cha A One Products &
Bottlers Recycle Unit cha Mbagala jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akipata ufafanuzi
kuhusu ukusanyaji wa chupa za plastiki kwa ajili ya kurejelezwa kutoka
kwa Balozi wa Global Youth Climate Network Bi.Neema Clarence alipokuwa
akitembelea kiwanda cha A One Products & Bottlers Recycle Unit
cha Mbagala jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...