Na Leandra Gabriel, Michuzi TV


BENKI ya dunia kupitia bodi ya wakurugenzi imeidhinisha kutolewa kwa mkopo wa dola za kimarekani milioni 500 (USD 500) kusaidia sekta ya elimu hasa kwa kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata na kumaliza elimu ya Sekondari salama na katika mazingira bora.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki ya dunia imeelezwa kuwa pesa hizo zitawanufaisha wanafunzi milioni sita na nusu wa shule za sekondari kwa kuisaidia Serikali kuanzisha mifumo madhubuti kwa wanafunzi walioacha shule katika mfumo rasmi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mkopo huo hutolewa wakati matokeo ya awali yamepatikana na hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza kwa idadi ya shule, kuboresha mifumo ya utolewaji wa elimu katika shule za umma pamoja na kuwasaidia watoto kuingia kwenye mfumo rasmi wa elimu ikiwa ataacha masomo.

"Kila mtoto nchini Tanzania anastahili elimu bora lakini wengi wanakosa fursa hii kwa kubadili maisha kila mwaka, mradi huu unawaweka vijana wa nchi hii mbele na kituo pamoja na kuweka mazingira bora na salama ya kujifunza kwa wasichana kwa kutoa theluthi mbili ya rasilimali" ameeleza  Mara Warwick ambaye ni Mkurugenzi mkazi wa Benki ya dunia nchini Tanzania.

Vilevile Warwick amesema kuwa Benki ya dunia itaendeleza mazungumzo na Serikali ya Tanzania juu ya masuala mapana ya malezi kwa watoto wa shule ili kuweza kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa sera ya elimu bure  ya Tanzania imepelekea watoto wengi zaidi kujiandikisha shule ambapo uandikishaji kwa shule za msingi umeongezeka kutoka watoto milioni 8.3 hadi milioni 10.1 kati ya mwaka 2015 na mwaka 2018 wakati uandikishaji kwa wanafunzi wa sekondari ukiongezeka kutoka milioni 1.8 hadi milioni 2.2 huku ikielezwa kuwaa licha ya kuboreshwa kwa viwango hivyo wanafunzi 60,000 sawa na asilimia 30 hushindwa kumaliza masomo yao kila mwaka.

Pia imeelezwa kuwa mradi huo utasaidia elimu bora ya sekondari ili kuhakikisha watoto wanafanikiwa hasa wasichana bila kujali hali na wanakuwa na njia ya kumaliza masomo yao ya sekondari, huku ikielezwa kuwa takribani watoto 300, 000 nusu yao wakiwa wanawake wameshindwa kuendelea na masomo ambapo kati yao 5500 huacha kutokana na sababu ya ujauzito.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...