Na Jumbe Ismailly IKUNGI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida
kimekamilisha zoezi la kutoa mafunzo kwa viongozi wa serikali za
vijiji,mitaa na vitongoji waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali
za mitaa na kutoa karipio kali kwa baadhi ya watu wanaotarajia
kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao
walioanza kujipitisha pitisha na kutoa rushwa kwamba majina yao
hayatasita kukatwa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ikungi,Bwana Mika
Likapakapa ametoa karipio hilo wakati wa kufunga mafunzo ya viongozi
wa serikali za vijiji yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya
sekondari Sepuka,kwa lengo la kukiimarisha na kuona uhai wa chama.

Alifafanua Likapakapa kwamba kitendo cha baadhi ya watu hao wanaoanza
kuingia kwenye maeneo na kuanza kufanya kampeni kabla ya muda kutokana
na aidha kuwanunua viongozi wa chama,kunaweza kuleta madhara ya
kukigawa chama hicho wakati wa uchaguzi ujao.

“Katika ziara hii tumeendelea kukemea sana baadhi ya watu wanaoingia
kwenye kata kufanya uharibifu wa kuanza kuwaona viongozi wa chama na
kutengeneza makundi ambayo yanaweza kukigawa Chama Cha Mapinduzi
(CCM).”alisisitiza Mwenyekiti huyo wa CCM.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo,vile vile CCM ilielekeza rungu kwa
baadhi ya watu wanaotoka nje ya Mkoa wa Singida na kwenda kuanza
kujitengenezea kura haramu majimboni kwa kuwatengeneza wapigakura ili
itakapofika uchaguzi waweze kuwapa kura.

“Kwa mfumo huo huo tumelikemea sana hilo ili kuweza kusimama wamoja
ili chama chetu cha mapinduzi tutakapoingia kwenye uchaguzi kusiwe na
makundi mengi ndani ya uchaguzi kwani athari ya makundi
yanaisababishia ccm kupoteza baadhi ya maeneo.”alifafanua mwenyekiti
huyo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Edward Mpogoro aliyekuwa mkufunzi mkuu
wa mafunzo hayo ya viongozi wa serikali za vijiji, alisema katika
kipindi cha siku sita walizokuwa katika ziara ya kutoa mafunzo
hayo,zaidi ya viongozi 2,340 kati ya 2,525 walipatiwa mafunzo ya
kutambua majukumu yao.

Hata hivyo Mpogoro alionyesha kutoridhishwa na asilimia saba ya
viongozi na wajumbe wa serikali za vijiji ambao hawakuweza kuhudhuria
kwenye mafunzo hayo ambayo yalikuwa ni muhimu kwao kutokana na ugeni
walionao katika uongozi baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza katika
uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita.

“Katika siku hii ya sita ya ziara yako Mh Mwenyekiti kitu gani Chama
Cha Mapinduzi kimefanya kwa ajili ya serikali yake na viongozi
wake,mpaka hivi leo Mh mwenyekiti,umetembelea kwa uwakilishi vijiji
vyote 101 vya wilaya yetu ya Ikungi na umekutana na viongozi wote wa
kata 28”.alisisitiza Mpogoro ambaye alikuwa mkufunzi mkuu wa mafunzo
hayo.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Singida magharibi,Elibariki Kingu
akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo hakusita kummwagia sifa lukuki
Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Edaward Mpogoro kutokana na utaratibu wake
alionao wakati wa ziara zake za kuwatembeklea wananchi na kusikiliza
kero zao.

Aidha Kingu alisisitiza pia kwamba licha ya awali kabla ya kuwa mbunge
alikuwa Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,lakini hakuwa na
utaratibu alionao Mpogoro wa kufanya ziara vijijini na kisha kulala
huko huko huku jioni akikutana na wazee kwenye vijiwe vya kahawa
kusikiliza changamoto walizonazo.

“Pamoja na wakati ule nilipokuwa DC nilikuwa nikiambiwa mkuu wa wilaya
kijana bora,lakini mimi nasema kwa dhati ya moyo wangu hata kama haupo
Mpogoro hili nitalizungumza,tunazidiana uwezo,dc huyu,huyu,huyu,huyu
ni mtu wa mungu na moja ni mnyenyekevu.”alifafanua Kingu.

Kwa mujibu wa Kingu sifa ya kwanza ya kiongozi,ukiona umechagua
kiongozi au ameteuliwa anaota mapembe,anatembea kwenye ac za serikali
anaona yeye ndio amemaliza na wananchi anawaona hamna kitu,ujue huyo
ametokana na mkono wa kushoto wa shetani,lakini Mpogoro ni
mnyenyekevu.

Hata hivyo Mbunge huyo kijana aliweka bayana sifa zingine za Mkuu wa
wilaya hiyo kuwa ni kujituma kwani katika kipndi kisichozidi miaka
miwili Mpogoro ameshatembea vijiji vyote vya wilaya hiyo,wakati Kingu
alipokuwa Mkuu wa wilaya hajawahi kulala Kijijini hata siku moja.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi,Mika Likapakapa(wa pili kutoka kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya shule ya sekondari Sepuka kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa viongozi wa serikali za vijiji wa Tarafa ya Sepuka.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Edward Mpogoro(wa kwanza kutoka kulia),Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi,Elibariki Kingu na Salumu Chima wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Sepuka(Hayupo pichani) akifungua mafunzo hayo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Ally Mwanga akiwasilisha taarifa fupi ya mafanikio yaliyopatikana katika Halmashauri hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.
Baadhi ya wenyeviti wa serikali za vijiji wa tarafa ya
Sepuka wakiahidi kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria,kanuni
pamoja na taratibu walizofundishwa na bila kumuonea mtu wala kutoa
upendeleo wowote.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...