Meneja wa TARURA wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Leopold Runji akitoa maelezo kwa mkuu wa Wilaya hiyo ,Mhe. Daniel Chongolo kuhusu miundombinu ya barabara katika makazi ya TBA muda mfupi baada ya kutoka kukagua mito inayochimbwa mchanga
Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo wakiwa wameshuka kwenye gari na kuelekea kwenye mto salasala kuangalia namna ya kuwadhibiti wananchi wanaochimba mchanga katika mto huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya walipofika kwenye mto salsala na kukutana na watu wakikimbia na chepe mara baada ya kuona msafara huo.
Wananchi waliokuwa wakichimba mchanga katika mto salasala.

************************************

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo ameliagiza Jeshi la Polisi Wilayani hapo kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuingia kwenyemito na kuchimba mchanga katika bonde la mto Salasala, bonde la mto Mbezi na bonde la mto Tegemeta.

Mhe. Chongolo ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na kushuhudia vitendo hivyo vikiendelea ikiwa ni takribani miezi miwili imepita tangu kuendesha zoezi la upandaji miti ya mianzi na magugu pamoja na kusitishwa kwa vibali vya uchimbaji wa mchanga viliyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu.

Amesema kuwa licha ya kutoa maelekezo pamoja na kusitishwa kwa vibali hivyo lakini bado wananchi wanaendelea kuchimba mchanga jambo ambalo amesema linahatarisha nyumba za makazi ya watu na hivyo kulisisitizia jeshi hilo kuwachukulia hatua wananchi hao ambao wanajihusisha na shuguli hizo.

“Tulishazuia hii mito isichimbwe mchanga, tumepita mto Salasala, Mbezi kule kwenye daraja la Malechela, pamoja na huku juu mpakani mwa eneo la jeshi la Lugalo, bado vitendo hivi vinaendelea nasisitiza naninaagiza jeshi la polisi kwenye Wilaya ya Mabwepande na Kawe ambayo ndio inahusika, niliagiza na leo narudia kwa mara ya pili hatutakuwa na msamaha kwenye jambo hili.

Amefafanua kuwa “mtu yeyote ambaye ataonekana analea vitendo vya uharibifu huu wa mazingira, tukimkuta na kumkamata tutamchukulia hatua kali za kisheria kwasababu jukumu letu sisi viongozi ni kusimamia na kuilinda sheria.

Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa“ Hatuko hapa kuwaonea watu, wala kuwaacha wananchi waharibikiwe na nyumba zao kwasababu ya maslahi na uroho wa watu wachache, kufanya hivi ni kuhujumu maslahi ya nchi hatuwezi kuendelea kuwaacha watu wanamna hii kwa hiyo nilazima tuchukue hatua kwa kila tutakaye mbaini anafanya shughuli hii.

Aidha Mhe. Chongolo amesema kuwa baada ya ziara hiyo ataunda timu ya kufuatilia mwenendo wa watu hao kwa kuwa alishatoa maagizo ya kuwashugulikia wote wanaohusika na kufanya shuguli za kuchimba mchanga kwenye mito hiyo.

Mapema mwaka huu, Mhe. Chongolo alisitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo.

Vibali vilivyositishwa ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi, Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo inapita katikati ya makazi ya watu na kwamba baada ya kufanyika marekebisho utawekwa utaratibu upya wa kufanya shughuli hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...