Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BHASHA  Mukherjee (24)  ambaye ni mlimbwende wa Uingereza mwaka 2019 amerejea katika fani yake ya udaktari na kurejea Uingereza akitokea India ili kusaidia waathirika wa virusi vya Corona ambavyo vimesambaa duniani kote.

Mukherjee alipewa taji hilo Agosti mwaka jana (2019) na kuchukua mapumziko katika fani yake yake ya udaktari na kujikita zaidi katika shughuli za kijamii na tayari amerejea Uingereza kutoka nchini India katika safari ya shughuli za kibinadamu.

Mrembo huyo aliyezaliwa Kolkata alikacha fani yake ya udaktari mara tuu baada ya kutwaa taji hilo kabla ya mlipuko wa virusi vya Corona kubadili maamuzi yake ambapo alinukuliwa akisema, "Haukuwa uamuzi mgumu" kwa yeye kurejea katika fani hiyo.

"Haukuwa uamuzi mgumu, nimekuwa Afrika, Uturuki na India ilikuwa nchi yangu ya kwanza kutembelea katika bara la Asia na nilikuwa na safari katika nchi nyingine ambazo kwa sasa nimezikatisha kutokana na mlipiko wa virusi vya Corona, na sehemu sahihi nzuri kwangu kwa sasa ni kurejea hospitali" Mukherjee aliieleza Fox News.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la CNN imeelezwa kuwa  Mukherjee amekuwa nchini India kwa wiki nne kabla ya mlipuko wa virusi vya Corona kuwa mbaya nchini Uingereza mwanzoni mwa mwezi Machi na alianza kupokea jumbe mbalimbali kutoka kwa watu wa karibu wakiwemo wafanyakazi kutoka hospitali aliyowahi kuhudumu na hakuona vyema kuendelea kuvaa taji hilo huku akifanya shughuli za kijamii wakati mamia ya watu wanafariki duniani na madaktari wenzake wanafanya kazi kwa bidii.

"Ninahitaji kurudi nyumbani, nikifika nitakwenda hospitali moja kwa moja" aliieleza CNN.

Mukherjee daktari bingwa wa masuala ya upumuaji amerejea nchini humo leo jumatano ili kuongeza nguvu katika kupambana na virusi vya Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...