Charles James, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo ameelezwa kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi na kuagiza kuongezwa kwa nguvu kazi.
Jafo ametoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya ukaguzi wa nyumba hiyo ambayo inajengwa na Suma JKT na kuwaagiza kuongeza nguvu ili Mkuu huyo wa wilaya aweze kuhamia katika muda uliopangwa.
" Nikiangalia idadi ya mafundi hapa na tarehe ambayo mmesema ujenzi utakamilika Mei 7 naona kabisa haitowezekana, sasa ili iwezekane ni lazima muongeze nguvu kazi na mbadilishe mpango kazi
Nataka Mei 8 DC wetu aingie kwenye nyumba yake, Suma JKT nyie ni taasisi ya serikali na tumewapa miradi mbalimbali hiyo maana yake tuna imani kubwa na nyinyi, hivyo niwasihi mfanye kazi hii kwa umakini na spidi inayotakiwa," Amesema Jafo.
Waziri Jafo pia amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino, Dodoma ambapo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
Hospitali ya Uhuru inajengwa baada ya Rais Dk John Magufuli kuelekeza fedha zilizokua zitumike kwenye sherehe za Uhuru mwaka 2018 zitumike kujenga Hospitali hiyo ambayo itakua msaada kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani ya Singida na Morogoro.
" Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi huu na hasa nimefurahishwa kwa kutekeleza maelekezo yangu niliyoyatoa ya kuongeza nguvu kazi. Sasa naona kuna idadi ya watu 300 kutoka 100 waliokuepo awali.
Niwatake viongozi wa Suma JKT mliopo hapa kusimamia vizuri ujenzi huu lakini pia kuongeza nguvu kwenye nyumba ile ya DC Dodoma, lengo ni kukamilisha kazi hizi katika muda uliopangwa," Amesema Jafo.
Pia Jafo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kufikisha vifaa vya ujenzi kwa wakati ili kutatua changamoto ya vifaa kutofika kwa wakati saiti jambo ambalo linaweza kufanya ujenzi kusikamilike kwa muda uliyopangwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akiwa kwenye nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Mafundi kutoka Suma JKT wakiendelea na ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Chamwino alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inajengwa wilayani Chamwino, Dodoma.
Mafundi zaidi ya 300 kutoka Suma JKT wakiendelea na ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani Chamwino.
Muonekano wa hatua za ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma kama inavyoonekana ambapo umefikia asilimia 25/
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...