Charles James, Michuzi TV
KIPI nakipenda? Ooh napenda mitazamo ya watanzania wenzangu pale wanapoamua kutoa maoni yao juu ya jambo Fulani. Leo watatoa maoni chanya kesho watatoa hasi. Twende taratibu.
Ni watanzania hawa hawa ambao walikua hawampendi Mjeshi wa Bongo Fleva, Harmonize kipindi akiwa lebo ya Wasafi inayomilikiwa na Supastaa, Diamond Platnumz.
Wabongo hawakumpa heshima Konde Boy, wengine wakasema anabebwa na promo ya Wasafi, wengine wakasema hakuna kitu yule anamuiga Diamond.
Mungu siyo Athuman, Harmonize akakua kimuziki, akajijenga kiuchumi akaomba kuondoka WCB, mambo yakawa mengi akalipa fedha ya kuvunja mkataba wake na maboss wake wa zamani.
Akajitoa na kuanzisha lebo yake, wale wale waliokua wanamponda wakaanza kumpa tano zao, ungewasikia " Sasa huyu ndio mtu wa kumpa changamoto Diamond, hakuna msanii kama Harmonize, kwanza ana hela balaa.
Sikiza. Wale waliokua wakimpenda kipindi yupo WCB wakageuza maneno, wakaanza kumtabiria mwisho mbaya, wengine wakasema anajiona kafika na hana shukrani kwa sababu Diamond ndio alimtoa kimuziki halafu leo anajifanya katoka anaondoka.
" Msanii gani yule bwana, hakuna kitu hizo fedha zenyewe za kununua mkataba kapewa na Sarah, hana lolote atafulia tu kwanza anamuiga Diamond, " Maneno ya wabongo ambao awali walikua wanamsapoti Konde.
Achana na ya Konde Gang. Tazama juzi wameanza kumshambulia Supastaa wa Soka, Mwana Samatta. Wananzengo wanasema imekuaje hatoi msaada kwenye janga hili la Corona.
Wameenda mbali zaidi wanasema huwa wanapoteza usingizi wao kumuangalia akiichezea Timu yake ya Aston Villa na wanampa sapoti kwa kuwa ni mtazania mwenzao.
Lakini wanashangaa kwanini hatoi misaada kusaidia wananchi na janga la Corona.
Watanzania hivi mnajua Samatta amepambana yeye mwenyewe kufika hapo alipo? Nyie mnaolaumu kwamba hatoi misaada mlimsaidia hata kununua njumu? Au ni kwa sababu bando ni lako hivyo hupangiwi cha kuandika Instagram?
Je una uhakika gani kwamba Samatta hajatoa michango? Pengine kwa sababu ya imani yake ameamua kutoa kimya kimya kwa wahusika bila kutangaza kwenye vyombo vya habari.
Huwa nacheka nikianza kufuatilia yanayoandikwa na wabongo wenzangu mitandaoni.
Sifa za mashabiki wa Simba kwa fedha za Bilionea Mohammed Dewji utafikiri na wao wana hisa pale. Katika kijiwe kimoja shabiki lialia wa Simba angetamba kwamba wao wana pesa ndefu na hakuna tajiri kama Mo.
" Sikiza wewe sisi ndio matajiri, Klabu yetu inaendeshwa na Bilionea no moja kijana Afrika, hakuna mchezaji tutamkosa tukimtaka, Mo ana pesa ndefu,".
Ni ukweli ulio wazi tangu Mo Dewji aanze kutoa noti zake pale Msimbazi, Simba wamerudi kuwa washindani haswa. Wametwa mataji mawili mfulululizo ya Ligi na wamefika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu jana.
Unakumbuka tweet ya Mo kutangaza kuachana na Simba baada ya kufungwa na Mtibwa Sugar kwenye fainali ya Mapinduzi Cup ile Januari?
Basi mashabiki wale wale waliokua wanajitapa nae, wale waliokua wakitambia fedha zake wakageuka, " Kwanza aondoke bwana Mo kitu gani walishapita matajiri kibao tu Simba na bado tulisonga.
Kwanza asitunyanyase sisi wenyewe tumemsaidia sana kukuza bidhaa zake toka aanze kutangaza na sisi. Asitutishe mbabaishaji tu yule."
Alivyotangaza kurejea tena mashabiki wale wale wakageuka na kuanza kumsifia, " Tulijua tu tajiri atarudi kwanza hawa wachezaji wanalipwa fedha nyingi ila wanamuangusha Mo,"
Hatujawahi kuwa na msimamo, tunayumbishwa na matukio kila siku. Hatujui tusimame wapi. Ni watu wa kusifia na kuponda yote yanayotokea. Hatuajwahi kuwa na 'way foward'.
Yanga! Waliyumba hapa katikati hadi kufikia kupitisha bakuli kwa mashabiki wao kutafuta fedha za uendeshaji. Wakapata wadhamini ambao ni GSM.
Mpunga ukaanza kunukia, wachezaji wakasajiliwa na wadhamini wao. Maneno yakaanza ya kuwapiga vita GSM kwamba wanaingilia kazi za viongozi.
Wadhamini wakaona isiwe shida tunajitoa. Kama ilivyokua kwa Mo wakati anajitoa ndivyo ilivyokua kwa Yanga. Na hata kurudi kwao stori ni ile ile.
Wabongo tunajuana! Wakipata tatizo ikatokea Mkuu wa Wilaya ameenda kutatua watashangilia sana na kusema bora amefika maana Mwenyekiti wao wa Mtaa hajawahi kuwasaidia hata kidogo.
Kesho akienda Mkuu wa Mkoa watasema DC hajawahi kuwasaidia, siku Rais akifika wataongea yaleyale na kusema hawajawahi kupata msaada wowote kwa viongozi wa ngazi ya wilaya na Mkoa. Unafiki ni jadi yetu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...