Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.

Manispaa ya Ubungo  imesema kuwa iko katika mkakati wa  upuliziaji dawa katika maeneo ya mbalimbali ikiwemo na sehemu za huduma za kijamii.

Akizungumza na Michuzi TV Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic Swai amesema kuwa mkakati huo ni kuchukua tahadhari ya kujikinga na Virusi vya Corona.

Swai amesema kuwa katika  kipindi chote hiki wananchi wazinagatie usafi wa kunawa mikono katika sehemu za huduma za Jamii kwani vifaa wameweka wameweka.

Amesema  katika upuliziaji huo wamepuliza katika vituo vya mabasi,Masoko likiwemo soko la Urafiki Mabibo yaendayo kasi vilivyopo katika Manispaa hiyo.

Aidha amewataka wananchi kuzingatia tahadhari ya Virusi vya Corona kwa kwa kuhakikisha wana nawa mikono katika kila sehemu wanazopita kupata huduma pamoja na kuepuka misongamano.

"Wananchi wa Ubungo wachukue tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Virusi vya Corona na kufuatilia taarifa za wataalam kuhusiana na ugonjwa huo"amesema Swai.


Upuliziaji wa dawa ukiwa unemaendelea katika Soko la Urafiki Mabibo'Mahakama ya Ndizi lililofanyika usiku wa Machi mbili , Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...