Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
RAIA na mwanajeshi wa zamani wa Brazili, Ermando Piveta, mwenye umri wa miaka 99, amekuwa Mbrazili mkongwe kupona maambukizi ya coronavirus na kuruhusiwa kutoka siku ya Jumanne.

Piveta aliyepigana vita ya pili ya dunia alitoka Hospitalini ya Kijeshi katika mji ya Brasilia hapo akiwa amevaa kofia ya jeshi na kusalimiana kutoka kwa kiti chake cha magurudumu akionesha ishara ya ushindi na kupigiwa makofi ya wahudumu wa hospitali hiyo.

"Kushinda vita hii ilikuwa kubwa kwangu kuliko kushinda vita," alisema juu ya mapigano yake dhidi ya adui asiyeonekana. "Katika vita unaua au unaishi. Hapa lazima upigane ili kuishi, ”akaongeza. 

Piveta alikuwa mjumbe wa pili katika Vikosi vya Jeshi la Brazil wakati wa Vita vya Kidunia vya pili na aliwahi kufika Afrika. Alipima virusi vya ugonjwa huo wiki mbili zilizopita na alikaa kwa siku mbili katika wodi ya wagonjwa mahututi ya hospitali baada ya kupata homa ya mapafu (pneumonia). 

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo ya Kijeshi amesema Piveta hakuwahi kupatikwa mashine ya kumsaidia kupumulia na ameweza kupona kutokana na umbo lake nzuri la mwili kutokana na maisha ya jeshi na maisha marefu ambayo yanaendesha katika familia yake.

Kuachiliwa kwa Piveta kutoka hospitalini umeonesha mwanga katika hali ya giza wakati janga hilo toka lishike kasi Brazili. 

Covid-19 imeambukiza watu 25,262 na kuwauwa watu 1,532, wizara ya afya ilisema Jumanne, na vifo vya watu 204 katika masaa 24 iliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...