Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa msaada wa Mabati yenye Thamani ya shilingi Milioni 476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000 za Wajane mkoani humo ambao nyumba zao zimeathiriwa na mafuriko yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amewataka Wananchi waliojenga mabondeni kuondoka.

RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua  na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.

Aidha RC Makonda amewapa siku 10 Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.

Aidha RC Makonda amesema athari zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba mikondo ya maji jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema kwa sasa serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja yaliyochukuliwa na Mafuriko ikiwemo ujenzi wa madaraja ya muda mfupi ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea.

RC Makonda pia amewaelekeza wakandarasi kutumia kipindi hiki cha mvua kuangalia kama Design ya madaraja wanayojenga yanakidhi kuhimili na kupitisha maji ya mvua ili wabuni design mpya zinazokidhi viwango.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda akitazama baadhi ya maeneo yalioathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini leo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua  na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda akitoa maelekezo kwa baadhi ya Waathirika (hawapo pichani)  wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua  na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.

 Pichani ni sehemu mbalimbali za nyumba zilizoathiriwa na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar na Kwingineko nchini
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...