Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii) kwa kushirikiana na Mtandao wa Malezi, Makuzi
na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN), Taasisi ya Chakula na
Lishe, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF)
wameandaa mkakati wa kufikisha ujumbe kwa watoto kuhusu kujikinga na
maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza leo katika kikao kazi kilichowakutanisha wadau hao jijini
Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Malezi, Makuzi na
Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN) Bruno Ghumpi amesema
kumekuwepo na ujumbe mbalimbali katika kujikinga na maambukizi ya
Virusi vya Corona ila kumekosekana ujumbe maalum unaolenga makundi
maaalum ikiwemo wanawake wajawazito na watoto wadogo kuanzia miaka 0 hadi minane.

Ameongeza kuwa kuwepo kwa elimu sahihi kwa watoto hao kuhusu ugonjwa
wa COVID 19 itawasaidia wazazi au walezi na watoto wenyewe kupata
taarifa zitakaziwasaidia kujikinga na Virusi hivyo ili kupunguza au
kuondokana na maambukizi ya Virusi hivyo katika maeneo yao.

“Ujumbe huu kwa watoto ni muhimu sana kwani kundi hili kwa sasa lipo
nyumbani kutokana na kufungwa kwa shule hivyo ni vizuri wazazi na
walezi wakazingatia masuala muhimu ya kuwafundisha watoto wao
kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona” amesema

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Bw. Mathias Haule amesema kuwa ni muhimu kwa wadau kuhakikisha
wanafikisha elimu katika ngazi ya chini kuanzia familia, kijiji/mtaa
ili kuwezesha watu hao kupata taarifa na elimu sahihi juu ya kujikinga
na maambukizi ya virusi vya Corona.

“Elimu ifike katika ngazi ya familia hasa katika maeneo ya vijijini
ambako bado elimu haijawafikia kwa kasi inayotakiwa ili kuondokana na
maambukizi ya virusi vya Corona nchini.” Amesema


  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN) Bruno Ghumpi (mwenye shati la batiki) akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa uwepo wa elimu kwa wazazi na walezi ili kuwaelimisha watoto kuhusu kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona katika kikao kilichofanyika jijini
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Iadara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Mathias Haule akichangia hoja katika kuandaa ujumbe utakaowalenga wazazi kuwaelimisha watoto jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao kilichowakutanisha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuandaa ujumbe utakaowalenga wazazi kuwaelimisha watoto jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...