Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (kushoto), akizungumza na Inspekta Jenerali wa
Polisi (IGP), Simon Sirro, wakati Mkuu huyo wa Jeshi alipoenda kuhani
msiba wa Baba Mzazi wa Waziri huyo, marehemu Boniface Simbachawene
Mwataguluvala, Kinyerezi Jijini Dar es Salaam, leo Aprili 17, 2020. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (katikati), akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ilala, Zubery Chembera (kushoto), alipokuja kuhani msiba wa baba mzazi
wa Waziri huyo, marehemu Boniface Simbachawene Mwataguluvala, Kinyerezi
Jijini Dar es Salaam, leo Aprili 17, 2020. Kulia ni Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP, Lazaro Mambosasa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya NchiM
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (wapili kulia), akimsikiliza Inspekta Jenerali wa
Polisi (IGP), Simon Sirro, wakati alipokuja kumfariji kwa kufiwa na baba
yake Mzazi, marehemu Boniface Simbachawene Mwataguluvala, Kinyerezi
Jijini Dar es Salaam, leo Aprili 17, 2020. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP),
Simon Sirro akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha baba yake Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (aliyesimama), jijini
Dar es Salaam, leo. Baba Mzazi wa Waziri huyo, Boniface Simbachawene
Mwataguluvala amefariki katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, jijini
Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Marehemu Boniface Simbachawene
Mwataguluvala, baba mzazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George
Simbachawene, ambaye amefariki katika Hospitali ya Benjamini Mkapa,
jijini Dodoma, leo.
*****************************
MHESHIMIWA
GEORGE BONIFACE SIMBACHAWENE, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAKE MZAZI, MZEE BONIFACE
SIMBACHAWENE MWATAGULUVALA (91) KILICHOTOKEA LEO TAREHE 17 APRILI, 2020
SAA 9:45 ALFAJIRI KATIKA HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA JIJINI DODOMA.
HABARI ZIWAFIKIE:
- FAMILIA YA MAREHEMU WALIOKO KIJIJI CHA PWAGA, WILAYA YA MPWAPWA, MKOA WA DODOMA NA WALE WALIOKO NJE YA MKOA.
- VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI, VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI, NA VIONGOZI WA VYAMA VINGINE VYA SIASA.
- NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI MBALIMBALI POPOTE PALE WALIPO.
MSIBA KWASASA UTAKUA SEHEMU ZIFUATAZO;
DAR ES SALAAM: NYUMBANI KWA MHE. WAZIRI, KINYEREZI.
DODOMA MJINI: NYUMBANI KWA NDUGU SEMGURUKA/MAMA DEVY – ILAZO.
KIBAKWE: NYUMBANI KWA MAREHEMU KIJIJI CHA PWAGA.
MWILI
UTASAFIRISHWA KUTOKEA DODOMA MJINI SIKU YA JUMAPILI
TAREHE 19/04/2020 BAADA YA IBADA FUPI ITAKAYOFANYIKA ILAZO. MAZISHI
YATAFANYIKA TAREHE 20/04/2020, SIKU YA JUMATATU NYUMBANI KWA MAREHEMU,
KIJIJI CHA PWAGA, JIMBO LA KIBAKWE, WILAYA YA MPWAPWA, MKOA WA DODOMA.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..AMINA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...