Jengo la ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) linavyoonekana baada ya ujenzi wake kukamilika na kisha kukabidhiwa rasmi leo Aprili 30 kwa Wakala huo Kanda ya Mashariki ili kuanza kutumika kwa shughuli mbalimbali za kiofisi.
 Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS),Kanda ya Mashariki Caroline Malundo(katikati) akisaini nyaraka za makabidhiano ya jengo la ofisi la TFS Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.Kushoto ni Mbunifu Majengo Majengo wa TBA-Pwani Greyson Kanyaburugo na kulia ni Mhandisi Bernard Lyimo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) Dar es Salaam.
 Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS),Kanda ya Mashariki Caroline Malundo(katikati), Mbunifu Majengo wa TBA-Pwani Greyson Kanyaburugo(kushoto na Mhandisi Bernard Lyimo(kulia) wakiwa wameshika nyaraka za makabidhiano ya jengo la ofisi la TFS Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani baada ya ujenzi wake kukamilika.
 Mbunifu Majengo wa Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) Mkoa wa Pwani Greyson Kanyaburugo(kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi jengo la ofisi la TFS Wilaya ya Mkuranga.Kulia ni Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Kanda ya Pwani Caroline Malundo akisikiliza kwa makini.
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Kanda ya Mashariki Caroline Malundo akisisitiza jambo wakati wa ukabidhiwaji wa jengo la ofisi la Wakala huo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

 Muonekano wa ndani wa jengo la ofisi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani baada ya ujenzi wake kukamilika na kukabidhiwa kwa Wakala huo.Jengo hilo limejengwa na Wakala wa Majengo Tanzania(TBA).
Baadhi ya watumishi wa TFS na TBA wakifuatilia maelezo ya ujenzi wa jengo la ofisi za TFS Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKALA wa Majengo Tanzania(TBA) umekabidhi jengo la Ofisi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani huku ikielezwa kukamilika kwa jengo sasa kunakwenda kuboresha shughuli za uhifadhi, utalii Ikolojiea na kukomesha uvamizi ndani ya msitu huo.

Jengo hilo lenye vyumba vya ofisi 14 limekabidhiwa leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani na kwamba hadi kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo jumla ya Sh.437,375,123.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kwa jengo hilo, Meneja wa TFS Kanda ya Mashariki(Dar es Salaam, Pwani na Morogoro) Caroline Malundo amesema chimbuko la mradi huo umetokana na uamuzi wa Wakala wa Huduma za Misitu kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo kwa ajili ya Meneja wa TFS Wilaya ya Mkuranga.

"TBA kupitia ofisi ya Meneja wa Mkoa wa Pwani ulipewa mkataba wa usanifu wa mradi huo na ofisi ya Meneja wa TBA Dar es Salaam alisani mkataba kama mkandarasi mkuu.Madhumuni ya mradi huo ni kumuwezesha Meneja wa TFS Wilaya ya Mkuranga kujitegemea katika majengo yake kutoka katika majengo ya kupanga.

"Pia kuwezesha watumishi wa TFS Wilaya ya Mkuranga kufanya kazi zao kwa ufanisi na tija wakati wa kuhudumia wananchi na misitu kwa kuwa na miundombinu bora na wezeshi,"amesema Malundo na kuongeza ujenzi wa jengo hilo ulianza mwaka 2018 na sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015.

Ameongeza kukamilika kwa jengo hilo pia ni kutekeleza mpango mkakati wa pili wa TFS huku akisisitiza dhumuni kuu la kujengwa kwa jengo hilo ni kuhakikisha Wakala huo unakuwa na jengo lake kwasababu walikuwa kwenye jengo la kupanga.

Hata hivyo amesema jengo hilo limejengwa ndani ya msitu wa Vikindu ili kuboresha na kuimarisha hifadhi ya msitu huo baada ya kuona kuna uvamizi uliokuwa unafanyika na kusababisha kuzorotesha nguvu kubwa ya uhifadhi.

"Hivyo uamzi wa kujenga jengo hili ulikuja baada ya kuona kuna haja ya kuboresha hifadhi yetu ya Vikindu, tunaamini uwepo wa jengo hili sasa uvavimizi wote uliokuwa unafanyika kwenye msitu huo utakoma.

"Pia utaimarisha utalii Ikolojia ambao umeanzishwa ndani ya msitu huo, hivyo tunawatangazia Watanzania kwamba ndani ya msitu wa vikundi kuna vivutio vya kutosha na hivyo mnakaribishwa kuja kuviona na kuongeza pato la Taifa,"amesema.
Kwa upande wake Mbunifu Majengo wa TBA -Pwani aliyemwakilisha Meneja wa TBA Greyson Kanyaburugo amesema kuwa wamekabidhi jengo hilo likiwa limekamilika kila kitu.

"Leo Aprili 30 mwaka huu tunakabidhi jengo hili la TFS Wilaya ya Mkuranga likiwa limekamilika,"amesema na kufafanua kuwa wamesaini nyaraka za uthibitisho wa makabidhiano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...