Na Karama Kenyunko globu ya jamii.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), imetoa tahadhari ya kunyesha kwa Mvua kubwa ndani ya siku nne kuanzia kesho Aprili 17, 2020.

Tahadhari hiyo imetolewa leo Alhamisi Aprili 16, 2020 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Kituo  Kikuu cha Utabiri wa Mamlaka hiyo, Samwel Mbuya  ambae amesema amesema mvua hiyo ya siku nne inatarajia kunyesha kuanzia ya April 17 hadi 20 mwaka huu.

Aidha ametaja maeneo yanayotarajia kupata vipindi vya mvua kubwa ni pamoja na Mkoa wa Pwani ,Kisiwa cha Mafia ,Tanga, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Amesema wanatarajia maeneo hayo kuwa katika hali ya tahadhari ya kupata  Mvua kubwa hususani siku ya Jumamosi na Jumapili pia amesem vipindi vya mvua kubwa zaidi zinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo hayo tajawa ambapo mpaka sasa maeneo hayo yanaendelea kupata vipindi vya mvua kubwa kwa takribani siku nne zilizopita na mvua nyingine inatarajiwa kunyesha kwa siku nne zijazo

Aidha Mbuya mewaasa wananchi kuchukua tahadhari zinazostahiki ili kupunguza athari ambazo zinaweza kujitokeza katika maeneo hayo na kuhakikisha wanazingatia maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika kuhusiana na ubora wa kupunguza madhara yanayoweza kutokea katika mvua hizi zinazotarajiwa kunyesha. Ame

Ameongeza kuwa, Mvua hizo nazo ni sehemu ya mvua za masika ambazo zilianza mwezi Machi mwaka huu na zinaendelea katika maeneo ya ukanda wa pwani na maeneo mengine nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...